KATIBU UWT WILAYA YA DODOMA MJINI ASAKA KURA ZA RAIS MAGUFULI KATA KWA KATA | Tarimo Blog

 


Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha Wilaya ya Dodoma inaongoza kwa kura za Urais wa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM, Umoja wa Wanawake Wilaya hiyo umefanya vikao vya ndani na wanawake wa kata za Makole, Chamwino na Kizota na kuwaeleza mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofikiwa na serikali ya Dk John Magufuli.

Akizungumza kwenye vikao hivyo, Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa amewaomba wanawake hao kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 wakiwa na vitambulisho vyao vya mpiga kura ili waweze kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde na madiwani wote wa kata 41 za Dodoma Mjini.

Madukwa amesema kwa miaka mitano ya Dk Magufuli wanawake wamenufaika na mikopo ya serikali inayotolewa kwenye Halmashauri zote nchini ambayo imekua haina riba wala makato yoyote jambo ambalo limewafanya kina mama wengi kupiga hatua za kimaendeleo.

" Dodoma sisi tumefaidika sana na Dk Magufuli kwanza ametuheshimisha kwa kuleta Makao Makuu ya Nchi hapa, wizara zote na taasisi ziko Dodoma hii ni fursa kubwa sana kwetu, ametujengea soko na stendi kubwa ambayo itakua chanzo cha mapato kwa Jiji letu, niwaombe Oktoba 28 mjitokeze kwa wingi mkapige kura.

Dodoma ya leo siyo kama ya zamani, miaka mitano nyuma tulikua hatuna barabara za lami tulizonazo leo, Dk Magufuli amepambana na changamoto zetu kwa kiasi kikubwa na amefanikiwa, tusimvunje moyo, tukampe kura nyingi za kishindo," Amesema Diana.

 Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akizungumza na wanawake wa Kata ya Makole alipofanya ziara ya kata kwa kata kuzungumza na wanawake wa Wilaya hiyo kwenye vikao vya ndani.

 Wanawake wa Kata ya Kizota wakimsikiliza Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa alipofanya kikao nao kuwaeleza mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kwenye awamu ya kwanza ya Rais Magufuli.

Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa (katikati) akimnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Madukani ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Devis Mwamfupe kwa wanawake wa Kata ya Madukani

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2