MAKAMBA AAHIDI KUFIKISHA UMEME VITONGOJI/VIJIJI HALMASHAURI YA BUMBULI AMBAVYO HAVIKUFIKIWA NA HUDUMA HIYO | Tarimo Blog

 

Mbunge Mteule wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba ameahidi kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo vijiji na vitongoji vya halmashauri ya bumbuli ambavyo  havijafikiwa na  umeme vitapatiwa huduma hiyo ili viweze kuondokana na changamoto hiyo .


Makamba alisema kuwa ilani ya chama cha mapinduzi CCM inaelekeza kuwa

maeneo yote ambayo hayajafikiwa na umeme yafikiwe ili  wananchi wa maeneo husika waweze kuondokana na  giza na wakae kwenye mwanga.


Alitoa ahadi hiyo  wakati wa Mkutano wa kampeni wa kutafuta kura za Rais

Magufuli na madiwani wa CCM uliofanyika kata ya Dule B na Mbuzii

 katika Jimbo la Bumbuli  Wilayani Lushoto.


Makamba aliwaomba wapiga kura wa jimbo hilo kutohadaika na wapinzani

wanaosema kwamba  CCM  hawajawaletea umeme kwani kila kitongoji kitapata nishati hiyo


"Hata Rais Magufuli anapopita huko mikoani kuomba  ridhaa

ya kuongoza tena ameendelea  kutoa ahadi hiyo ya kusambaza  umeme katika nchi nzima hasa maeneo ambayo hajafikiwa  hivyo  October 28 jitokezeni kumpa kura nyingi ili aweze kutimiza ahadi hiyo"alisema Makamba.


Alisema kuwa  dalili  yakwamba  umeme utafika maeneo yote  tayari

baadhi ya nguzo zinaoneka  tofauti na miaka mitano iliyopita  hakukuwa na

nguzo hata moja hivyo endeleeni kuiamini CCM katika miaka mitano ijayo ili iweze kumalizia  changamoto zilizopo na ahadi zake


Mbali na umeme Makamba aliahidi  uboreshaji wa miundombinu mingine ikiwemo uboreshaji wa shule za msingi na sekondari  katika miaka mitano  ijayo lengo likiwa  ni kuweka mazingira bora  ya kujifunzia wanafunzi ili kuwapa hamasa ya kuongeza ufaulu katika masomo yao


" Mchagueni Magufuli  kwa kura nyingi za kishindo ili mnipe nguvu mimi na

diwani wenu ili tutakapoenda kuomba majawabu ya changamoto zetu iwe rahisi kusikilizwa "alisema Makamba ambaye anaendelea na kampeni Kijiji kwa Kijiji  kuhakikisha CCM imashinda kwa kishindo


Hata hivyo alisema kuwa Mgombea wa CCM ambaye anamaliza kipindi chake cha awamu ya kwanza ya  Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani licha ya kufanya mambo mengi ya kimaendeleo lakini pia amefanikiwa pia kurudisha nidhamu katika utumishi wa umma na kurudisha  chachu mpya ya Watanzania ya kujitafutia Maendeleo.


Alisema kuwa Chama cha mapinduzi kimefanya  mengi na kimetekeleza  kwa

kiasi kikubwa  ahadi nyingi walizoahidi 2015 japo bado changamoto zipo

lakini asipite mtu kuwadanganya kwamba atamaliza changamoto zote kwani tangu Dunia iumbwe hakuna mtu aliyewahi kumaliza changamoto zote

Mbunge Mteule wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba  alipokuwa akizungumza  wakati wa Mkutano wa kampeni wa kutafuta kura za Rais Magufuli na madiwani wa CCM uliofanyika kata ya Dule B na Mbuzii

 katika Jimbo la Bumbuli  Wilayani Lushoto.




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2