SERIKALI: TUMEWEKA MAZINGIRA WEZESHI NA TENDAJI KWA NGOs NCHINI | Tarimo Blog



Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo
ya Jamii Vickness Mayao ambaye pia ni Msajili wa NGOs akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Ofisi ndogo za Shirika la Foundation For Civil
Society Jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Vickness Mayao ambaye pia ni Msajili wa NGOs akikata utepe
kuashiria ufunguzi wa Ofisi ndogo za Shirika la Foundation For Civil
Society Jijini Dodoma.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

SERIKALI imesema, imeweka mazingira wezeshi ya utendaji wa Mashirika
yasiyo ya kiserikali nchini zikiwemo Sheria, Kanuni, miongozo na
taratibu mbalimbali zitakazowezesha kuwa na uratibu na usimamizi
mzuri.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Vickness Mayao wakati akifungua
Ofisi ndogo za Shirika la Foundation For Civil Society mkoani Dodoma.

Aidha, Vickness amesema pamoja na kuyawekea Mashirika mazingira
wezeshi, Serikali kwa kushirikiana na wadau imepitisha mwongozo wa
uratibu wa pamoja wa Mashirika hayo na kupitia mwongozo huo Mashirika
sasa yanaelekezwa kushirikiana na Sekta mbalimbali katika kutekeleza
majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuzingatia vigezo vya kitaalamu.

Vickness ametoa rai kwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na wadau
wengine kutumia fursa ya kufungua Ofisi katika makao makuu ya nchi
vizuri kwa maslahi ya mapana ya nchi yetu na maendeleo ya Sekta ya
Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Ameongeza kuwa amefurahishwa na Shirika hilo kwa kufungua Ofisi hiyo
ambayo pia itatumika kama kituo cha Asasi za Kiraia jijini Dodoma na
kitatumika kama kituo cha taarifa, ushauri, maarifa na mahali pa
kufanyia kazi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo, wana
Azaki, Asasi za kijamii, Serikali, sekta binafsi, Taasisi za kitaaluma
na utafiti pamoja na jumuiya za kimataifa ili kuwezesha wananchi
kupata, kutumia na kujifunza shughuli za Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali nchini.

"Napenda kuchukua nafasi hii kulipongeza Shirika la Foundation For
civil Society na Mashirika mengine yaliyoona umuhimu wa kufungua Ofisi
zake hapa Dodoma." amesema.

"Hili litatekelezwa vizuri endapo Mashirika yatapata fursa ya kupata
taarifa sahihi na maarifa kupitia vituo vya kutoa taarifa kama hiki."
ameeleza.

Pia amesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano, uwazi na
uwajibikaji na kujengeana uwezo kati ya Mashirika yasiyo ya kiserikali
ili kufikia maendeleo endelevu

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2