Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
TAASISI ya Habari Development Association imekutana na waandishi wa habari kwa lengo la kukumbushana wajibu wao katika kukemea kauli zisizokuwa za kujenga Taifa zinazotolewa na baadhi ya wagombea wa Urais hususan Tundu Lissu ambaye anakiwalisha Chadema.
Imesema Lissu amekuwa akitoa kauli zisizokuwa za kiungwana na zenye kujenga mpasuko mkubwa kwa Taifa ikiwemo ya kujitangaza kuwa ni mshindi halali wa Urais akiwa katika kampeni zake katika Mkoa wa Geita na mikoa mingine mbalimbali ya Mara, Shinyanga na Mwanza.
Taarifa ya Taasisi hiyo waliyoitoa leo Septemba 30,2020 kwa vyombo vya habari imesema kuwa Lissu pamoja na viongozi wenzake wamekuwa wakitoa mastamshi ambayo taasisi hiyo inaona ni matamshi yasiyoijenga Tanzania bali yapo kwenye tafakuri ya kuleta mpasuko kwa jamii.
"Tunaona na tunaamini vitendo na kauli anazotoa Tundu Lissu sio nzuri na zinazusha taharuki kubwa kwenye jamii hasa wakati huu ambao nchi iko kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.Sisi Taasisi ya Habari Development tunaiomba Tume ya Uchaguzi Nchini (NEC) kusimama na kutoa kauli kulingana na sheria za uchaguzi kuwa vitendo anavyovifanya Lissu sio vizuri na vipo katika misingi ya kuleta mpasuko kwenye jamii.
"Tunaamini huu ni wakati wa kila mwandishi wa habari kuwa imara na kupinga kauli hizi au kuvipuuza vitendo hivio ambavyo vina lengo la kuibomoa nchi na kuteteresha amani ya Tanzania ambayo imejengwa kwa nguvu kubwa,"imesema taarifa hiyo.
Taasisi hiyo kupitia taarifa hiyo imeongeza kila mwanasiasa anapaswa kuilinda amani na achunge ndimi zake kwa kuwa uhuru na amani ilioko ni tunu kubwa na anapokuja mwanasiasa anayesema kuwa yeye ndio mshindi kwa kigezo cha kujaza watu katika mkutano mmoja si jambo nzuri na tunalikemea kwa nguvu zote.
Pia imesema kuna umuhimu mkubwa wa kukemewa suala hilo na wanaiomba NEC kuchukua hatua kwa mgombea yeyote anayekwenda kinyume na taratibu za nchi kwa kuwa vitendo na kauli wanazotoa zinahatarisha amani.
"Kutokana na hali hiyo, Taasisi ya Habari Development Association tunamsihi na kumuomba Tundu Lissu afahamu ana dhamana kubwa ya usalama wa nchi yetu ambayo yeye kama mgombea tunamuomba amwage sera zake na jukumu la nani mshindi litatolewa na Tume ya Uchaguzi baada ya wananchi kumaliza kupiga kura,"imesema taasisi hiyo.
Pamoja na hayo imefafanua kama mjuavyo hivi
sasa nchi yetu ipo kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambao ni takwa la kikatiba na kidemokrasia kila ifikapo miaka mitano, nchi inafanya uchaguzi mkuu, hivyo huu ni wakati muhimu na waandishi wa habari kama wadau ni wakati wao kujitafakari kwa kuitumia vyema kalamu yetu kuelekea uchaguzi mkuu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment