WAZIRI BASHUNGWA AKAGUA UJENZI WA KIWANDA CHA MAZIWA KARAGWE | Tarimo Blog

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (mwenye shati
nyeupe) akikagua ramani ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa cha
Kahama Fresh kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata Lita 10,000 kwa
mzunguko mmoja na gharama za ujezi mpaka kukamilika ni Billioni 2.4,
kiwanda hicho inachojengwa eneo maalum la viwanda lililopo Kihanga, Wilaya ya Karagwe, Mkoani Kagera. Kulia ni mkandarasi wa ujenzi, Projestus Mwemezi wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kahama Fresh, Jossam Mtangeki.
   
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia)
akimpongeza Mkurugenzi wa Kahama Fresh Limited, Jossam Mtangeki  kwa
kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa cha Kahama
Fresh kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata Lita 10,000 kwa mzunguko
mmoja na gharama za ujezi mpaka kukamilika ni Billioni 2.4,
kinachojengwa eneo maalum la viwanda lililopo Kihanga, wilaya ya
Karagwe, Mkoa Kagera.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (mwenye shati jeupe) akikagua eneo unapofanyika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata
maziwa cha Kahama Fresh kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata Lita
10,000 kwa mzunguko mmoja na gharama za ujezi mpaka kukamilika ni
Billioni 2.4, kinachojengwa eneo maalum la viwanda lililopo Kihanga,
wilaya ya Karagwe, Mkoa Kagera. Kulia kwa Bahungwa ni Mkurugenzi wa
Kahama Fresh, Jossam Mtangeki.
Eneo unapofanyika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa cha Kahama
Fresh kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata Lita 10,000 kwa mzunguko
mmoja na gharama za ujezi mpaka kukamilika ni Billioni 2.4,kiwanda hicho
kinachojengwa eneo maalum la viwanda lililopo Kihanga, Wilaya ya
Karagwe, Mkoa Kagera.(Picha zote na Eliud Rwechungura.) 
*Aagiza Katibu mkuu na Taasisi kufika kiwandani hapo

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,  Innocent Bashungwa amemuagiza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe
kufika kwenye kiwanda cha maziwa kinachojegwa kihanga, Karagwe ili
kutatua changamoto anazozipata Mwekezaji wa kiwanda hicho.

Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo leo Oktoba 03, 2020  alipotembelea
na kukagua ujenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa cha Kahama Fresh
kinachojengwa eneo maalum la viwanda lililopo Kihanga, Wilaya ya
Karagwe, Mkoani Kagera.

“Namuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kufika hapa
Kihanga Karagwe kwenye kiwanda cha maziwa kinachojengwa, akiambatana
na Idara ya Maendeleo ya Viwanda na taasisi za NARCO, TIC, EPZA,
TARDB, TANESCO pamoja na taasisi nyingine Katibu Mkuu atakazoona
Zinafaa kumsaidia mwekezaji ili kuhakikisha kiwanda hiki hakikwami.”
amesema Bashungwa.

Waziri Bashungwa amepongeza jitihada za mwekezaji mzawa wa Kahama
Fresh Limited, Bwana Jossam Mtangeki kwa kusaidia utekelezaji wa dira
Serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi wa viwanda maana kwa
mkoa hapakuwa na kiwanda cha maziwa chenye ukubwa wa kuchakata lita
10,000 kwa siku.

Sambamba na hayo, Waziri Bashungwa amefurahishwa na mpango wa uwekezaji ambapo kutakuwa na kiwanda kinachotengeneza vyakula vya     ng’ombe wa maziwa, Pia amepongeza kwa kuwepo kwa shamba la ngo’ombe wa mfano ambalo linawasaida wafugaji wadogo kupata elimu ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

Aidha, Waziri Bashungwa amejadiliana na mwekezaji  mpango wa kugawa
ngo’ombe kwa wafugaji wadogo wadogo na namna ya kuwasaidia wafugaji
hao ili kupitia Serikali, Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara na
wizara ya Kilimo ziweze kuwaweka hao wafugaji wadogo wadogo katika
mfumo wa ushirika ili huduma za vyakula vitakavyozalizwa na kiwanda
hicho viweze kuwafikia kupitia ushirika wao, ili serikali kupitia
taasisi zake ziweze kuwasaidia wafungaji hao wa ng’ombe za maziwa
ndani ya wilaya karagwe ili waweze kuuza maziwa yao kwenye kiwanda
kinachoendelea kujengwa.

Mkurugenzi wa kampuni ya Kahama Fresh Limited, Jossam Mtangeki
ameishukuru Serikali Kupitia Waziri wa Viwanda na Biashara kwa
kuendelea kuwewekea mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kutenga maeneo
maalum ya viwanda kwa kila wilaya na kuwasogezea mahitaji muhimu
ambayo yanahitajika katika uwekezaji wao.

Jossam wakati akitoa taarifa ya kiwanda kwa Waziri Bashungwa amesema
kuwa ujenzi wa kiwanda hicho umefikia kiwango cha kujenga majengo ya
ofisi na kusawazisha eneo kitakapojegwa kiwanda na kiwanda
kitakamilika ndani ya miezi sita na kitakuwa na uwezo wa kuchakata
Lita 10,000 kwa mzunguko mmoja na gharama za ujezi mpaka kukamilika ni
Billioni 2.4

Aidha, Jossam ametoa wito kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kuitumia
fursa hiyo ya kiwanda hicho kukabiliana na changamoto ya soko la
maziwa ambalo lilikuwa ni tatizo la muda mrefu, ambapo amewaomba
wafugaji wa mkoa kagera kujikita na kuendelea kufuga ng’ombe wa maziwa
kwa tija ambao utasaidia kiwanda hicho kufanya kazi pia na wao
kunufaika kupitia uwepo wa soko la uhakika la maziwa kupitia kiwanda
hicho.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2