*Aahidi kuanzisha Diwani Fund ya kukopesha wananchi wake bila riba
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
WANAFUNZI wenye changamoto za kiuchumi za kifamilia zinazosababisha kushindwa kusoma kwa kukosa Vifaa mbalimbali katika kata ya Mzimuni zimeweza kutatuliwa na Diwani wa Kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto alifanya jitihada za kutoa daftari na Kalam ambapo kumeibuka uwepo wa wahitaji wengi kuliko alivyofikiri.
Vifaa hivyo zimenufaika shule ya za Msingi na Sekondari katika kata hiyo na zaidi ya wanafunzi 50.
Manfred Lyoto ni wa Diwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo vifaa hivyo ilikuwa ni sehemu ya kushughulikia changamoto ya elimu.
Wanufaika wa msaada huo hasa walezi wa watoto hao walisema kuwa wanampongeza Diwani huyo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto wao kwani uhitaji wa vifaa hivyo ulikuwa ni mkubwa na kwamba wakati watoto wao au majukumu walitaka kufunga shule walikuwa na changamoto hiyo.
"Hapa tulipofika sasa ndio ameanza kutekeleza ahadi zake hivyo tunamuomba Mhe. Diwani wakati mwingine atusaidie hata mabegi na sale za shule kwani hali wetu kifedha sio nzuri kutokana na changamoto mbalimbali za wazazi na walezi" amesema mmoja wa wazazi wa watoto Fatuma Kaloli.
Amesema majukumu wake alitelekezwa na baba yake hivyo jukumu la kumlea analo yeye tangu anaanza chekechea hadi sasa yupo darasa la saba huku mama mzazi akiwa amepata changamoto ya ukiziwi.
Naye mzazi mwingine Tabu Adamu, alitoa pongezi kwa msaada huo na kuwa ni wakati mwafaka kwa wadau wengine kuona umuhimu wa kujitokeza kuwasaidia watoto wasiokuwa na uwezo wa vifaa hivyo vya shule na si kumwachia Diwani peke yake.
Diwani Lyoto akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kutokana na kwamba alipata taarifa ya kuwepo na watoto wenye uhitaji wa vifaa hivyo kutokana na wazazi wao kutokuwa na kipato cha kujitosheleza kwani wengi hasa akina mama walimfuata na kumwelewa kuwa wana changamoto hiyo kwa ajiri ya watoto wao.
Amesema mwezi Januari alikuwa anafuatwa na wazazi na walezi kuomba msaada na ndipo akamua kuanzisha utoaji wa vifaa kupitia shule.
Lyoto amesema japokuwa nimepata taarifa kumbe kuna watoto wengine hawana hata mabegi wala sale za shule na kuahidi kushughulikia.
"Masuala yote nimeyachukua kutokana na kwamba huu ndio mwanzo lakini pia kuna mfuko wa Diwani (Diwani Fund), ambao unaanzishwa mda si mrefu ambapo wafanyabiashara ndogo ndogo watakuwa wanakopeshwa bila riba lengo likiwa ni kuwafanya wajikwamue na umaskini lakini pia mwisho wa siku waache kuwa tegemezi," alisema.
Watoto waliopewa msaada huo wapo yatima, wasiokuwa na wazazi na wale waliotelekezwa ambapo pia Diwani huyo alisema kuwa watoto hao kwa Kata nzima kwa uchache huo ataendelea kutoa msaada zaidi ili kuhakikisha wanafikiwa wote kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine huku suala la chakula mashuleni likiendelea kufanyiwa kazi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment