Na Woinde Shizza, Michuzi Tv -ARUSHA
WITO umetolewa kwa halmashauri hapa nchini pamoja na mamlaka ya mapato (TRA) kufanya kazi usiku na mchana ili kuweza kupunguza wizi wa mapato unaofanywa na baadhi ya watu wasio na nia njema na serikali, pamoja na kuhakikisha wanakomesha ukwepaji wa ulipaji kodi ya mapato.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karatu John Lusian Mahu wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya baadhi ya wananchi ambao sio waaminifu wanavyoiibia serikali mapato kwa kutorosha vitu usiku.
"Kwa mfano kwenye Wilaya yetu kuna watu wanaenda kuchota mchanga usiku malori kwa malori wakitegemea saa hizo hakuna mtu anayewatoza ushuru na kwakweli wanafanikiwa kwa hilo, vilevile Kuna uvushaji wa samaki kwa sababu sisi tunaziwa linatoa samaki kule Eyasi wanatoroshea upande wa Singida kwa sababu ya gari kutembea usiku na kufikisha katika masoko na hao ndio wakwepaji wakuu wa ushuru."Aliasema.
Alisema kuwa wajanja wachache wamekuwa wakitorosha bidhaa ambazo zinapaswa kulipishwa ushuru ambapo wamekuwa wakisafirisha usiku wakitegemea nyakati hizo hakuna mtu anayeweza kuwakamata na kuwadai ushuru.
Alisema wakwepaji wa ushuru katika halmashauri ni wengi sana hivyo ni vyema serikali ikaingilia kati na kuwatafutia walinzi wakiwepo mapolisi kwa sababu halmashauri hazina polisi ambao wafanya kazi ya kukamata wezi hao ambao wanatorosha vitu bila kulipia ushuru.
Aidha aliwataka pia watu wa mamlaka ya mapato Tanzania kuongeza muda wa kufanya kazi na ikiwezekana wafanye kazi usiku na mchana Ili kuweza kuzuia watu hao wanaolirudisha taifa nyuma kwa kupoteza mapato kwa makusudi kabisa.
"Unajua Kama bandarini wameweza kufanya kazi usiku na mchana yaani masaa 24 kwanini halmashauri zetu zisiweze kufanya kazi usiku na mchana na kuweza kuokoa fedha hizo ambazo zinaibiwa na watu wachache wasio wazalendo kwa nchi yao." Alisema John.
Aliwataka wananchi kuwa waaminifu na kuacha kuiiibia serikali kodi kwani fedha ambazo wanazitoa, zinasaidia kuletea maendeleo ikiwemo ikiwemo huduma za kijamii Kama vile barabara,shule,hospitali, miundombinu ya maji pamoja na mambo mengine.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment