KAMATI YA UONGOZI MKURABITA YAANZA ZIARA YA UFUATILIAJI NA UTEKELEZAJI SHUGHULI ZA URASIMISHAJI ARDHI NA BIASHARA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI | Tarimo Blog

 Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) inaanza ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa ardhi na biashara katika mikoa ya  nyanda za  juu kusini.

Akieleza kuhusu ziara hiyo Jijini Dodoma katika mahojiano maalum yaliyofanyika Januari 23, 2021, Mratibu wa Mpango huo, CPA, Dkt. Seraphia Mgembe amesema kuwa kamati hiyo itashiriki katika kazi mbalimbali ikiwemo zoezi la utoaji hati za hakimiliki za kimila za kumiliki ardhi katika halamshauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya masjala ya ardhi katika Kijiji cha Kapya wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Akieleza zaidi kuhusu ziara hiyo Dkt. Mgembe amesema kuwa ziara hiyo ya wiki moja inaanza leo Januari 24, 2021  hadi Januari 31,2021.

MKURABITA imekuwa ikiwezesha wanachi kipitia urasimishaji ardhi na biashara katika halmashuri mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mratibu wa Mpango huo, CPA, Dkt. Seraphia Mgembe



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2