MARUFUKU KUWARUDISHA WANAFUNZI MAJUMBANI | Tarimo Blog



Na Woinde Shizza, Michuzi TV-Arusha 
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru  Emmanuel Mkongo amepiga marufuku walimu wakuu, wakuu wa Shule, watendaji Kata na Vijiji kuwarudisha nyumbani Wanafunzi ambao Wazazi wao hawajatoa
michango ya Chakula na Katarasi ambayo  wamekubaliana kwenye Vikao
kamati za shule, bodi za Shule, Halmashauri za Vijiji na mikutano
mikuu.
Rai hiyo imetolewa  baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya
wananchi na wazazi kulalamikia vitendo vya wanafunzi kurejeshwa
majumbani kutokana na  wazazi wao kutokutoa michango .

Mkongo amesema, Halmashauri hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali za
kinidhamu walimu  au watendaji watakaohusika  kuwarudisha nyumbani
Wanafunzi kwa sababu za michango kwani kufanya hivyo ni kinyume na
maelekezo ya Waraka wa Elimu Na. 3 wa mwaka 2016.

Mkongo ametoa agizo hilo  wakati wa Mkutano na 
Madiwani wa Kata ya Mbuguni na Shambarai Burka, wenyeviti wa vijiji,
wenyeviti wa vitongoji, wajumbe wa Halmashauri za vijiji, watendaji wa
Kata na vijiji, walimu na waratibu Elimu wa Kata hizo uliofanyika
katika ukumbi wa  ofisi za Tarafa ya Mbuguni.

Ikumbukwe kuwa  Serikali imekuwa ikitoa fedha kwaajili ya utoaji wa
Elimu Bila Malipo katika shule za Sekondari na Msingi katika
Halmashauri ya Meru.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2