RC ARUSHA AAGIZA TRA NA TAKUKURU KUFUATILIA WOTE WANAOSTAHILI KULIPA KODI | Tarimo Blog


Mkuu wa mkoa wa Arusha  Iddi Kiman'ta (wa pili kushoto) akiwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC)wa kwanza kushoto katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega na wa kwanza kulia ni mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro  Rashid Mfaume akifuatia na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven.


 Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -ARUSHA

Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Hassan Kimanta ameiaigaza mamlaka ya mapatao  mkoani humo(TRA) kwa kushirikiana na Tasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwafuatilia watu wote wanaostahili kulipa kodi na kuhakikisha wanalipa.

Kimanta ametoa agizo hilo leo wakatiakifungua kikao cha kamati ya
ushauri ya mkoa (RCC) ambalo alisema kuwa ukusanyaji wa kodi ni lazima
upewe kipaumbele katikat mkoa huo ili maendeleo yaweze kupatikana
katika sekta zote.

Amesema kuwa wakikusanya kodi kwa wingi wanaijengea serikali uwezo wa
kutengeneza miundombinu ya vituo vya afya, barabara, maji shule na
mengineyo hivyo wale wote wanaostahili kulipa kodi ndani ya mkoa wa
Arusha walipe.

“Natoa maelekezo kwa meneja wa TRA mkoa wa Arusha ashirikiane na
Kamanda wa TAKUKURU mkoa kuwafuatilia wote wanaostahili kulipa kodi na
kuhakikisha wanalipa, tunataka kodi.”Amesema Kimanta.

Amefafanua kuwa hakuna haki bila wajibu hivyo ukusanyaji wa kodi ni
lazima, kwani ikilipwa wanaijengea serikali uwezo wa kutoa huduma
stahiki kwa wananchi.

Aidha kwa upande wa elimu amesema kuwa, Mkoa wa Arusha unaongoza kitaifa ambapo katika matokeo ya kidato cha nne na kidato cha pili imeongoza kitaifa  huku upande wa afya ukiwa ya pili kwa suala la lishe ikifuatiwa na kigoma.

Ameeleza mafanikio hayo yametokana na mshikamano mkubwa walionao
unaowafanya wafanikiwe na kuwasihi viongozi wa sekta
zote kuendeleza mshikamano huo kwa kuwa wamoja, kupendana  na kushirikiana katika kutatua changamoto.

Amesema katika wilaya zote sita Kuna upungufu wa madarasa  126 ambapo
amewashukuru wakuu wa wilaya na wakurugezi kwa kazi kubwa
wanayoendelea kuifanya kuhakikisha ya kujenga madarasa kwa
kushirikiana na wananchi na hadi kufika Februari 28 upungufu huo
utakuwa umeondoka.

“Lazima madarasa yajengwe na ni lazima kasi iongezeke ili pasiwepo na
wanafunzi watakaoshindwa kusoma Kutokana na ukosefu wa miundombinu ya madarasa.” Alisema Kimanta.

Amesema Mkoa wa Arusha mpaka sasa upo shwari na vyombo
vya usalama vinatekeleza wajibu wake kutatua changamoto ndogo ndogo
zinazojitokeza .

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2