SHULE YA SANINIU LAIZER YAANZA MASOMO YA MCHEPUO WA KIINGEREZA | Tarimo Blog

 

Mwalimu Swedefrida Musoma akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza na awali wakiwa shuleni kuendelea na masomo yenye mchepuo wa kiingereza katika shule ya Saniniu Laizer (picha na Woinde Shizza, ARUSHA.)


Na Woinde Shizza, Michuzi Tv Arusha


SHULE ya Saniniu Laizer iliyojengwa na mchimbaji mdogo wa Madini ya Tanzanite, katika Kijiji cha Naepo , wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara imeanza kufundisha rasmi ya baada ya kusajili wanafunzi wapatao 251 wa darasa la awali na la kwanza .

Shule hiyo imesajiliwa kama shule yenye mchepuo wa kiingereza baada ya serikali kukubali ombi la Laizer aliotaka serikali kuifanya shule hiyo iwe ya mchepuo wa kiingereza ili kuisaidia jamii ya Wafugaji kuelewa lugha ya kiingereza.

Akiongea na vyombo vya habari shuleni hapo Jana, Laizer alisema kuwa shule hiyo tayari imepata UsajiLi wa kudumu  na imesajiLi wanafunzi zaidi ya 250 wa darasa la Kwanza na awali.

Laizer ameishukuru serikali kwa kukubali ombi lake la kuifanya  shule hiyo iwe ya mchepuo wa kiingereza kutokana na maeneo ya Wafugaji kutokuwa ya huduma ya elimu hiyo na kusababisha wengi wao kutojua lugha ya kiingereza.

"Tunaishukuru serikali kwa kukubali shule hii iwe ya mchepuo wa kiingereza kwani jamii ya wafugaji haikuwa na shule ya kiingereza
Na hii itakusaidia watoto wetu kujua lugha ya kiingereza." Alisema

Alisema kwa Sasa anajipanga kujenga bwalo la kisasa la chakula litakalogharimu kiasi cha sh. milioni 45 ili kuwasaidia wanafunzi hao ambao ni wadogo waweze kusoma na kula chakula shuleni hapo.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo, Swedefrida Msoma alisema kuwa shule hiyo ilizinduliwa rasmi januari 13 Mwaka huu baada ya kukabidhiwa serikali.

Alisema shule ya Saniniu Laizer ilianza kupokea wanafunzi januari 18  Mwaka huu na kwamba hadi sasa ina jumla ya wanafunzi wapatao 251 na walimu wawili .

Alisema changamoto kubwa kwa Sasa ni wanafunzi kuchelewa kufika shuleni kutokana na umbali wa makazi yao.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2