SITAKI KUONGOZA WILAYA WANANCHI WAKE HAWALIPI KODI-DC MTWARA. | Tarimo Blog


 Na Mwaandishi Wetu Mtwara

MKUU wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amesema hataki kuongoza wilaya ambayo wananchi wake hawatoi kodi huku akisisitiza wote wanaodaiwa kodi ya ardhi kulipa madeni yao ifikapo  tarehe 30 mwezi huu.

Kyobya amesema hayo wakati akiongea na wadawai sugu wa kodi ya ardhi manispaa ya Mtwara Mikindani. Amesema kumekuwepo na madeni ya zaid ya shilingi bilioni 3 yanayotokana na kodi ya ardhi kutoka kwa taasisi za serikali, za dini na watu mbalimbali ambao hawalipi kodi zao kwa muda mwafaka.

“Tumewaita hapa ili tujadili na kukubalina namna bora ambayo madeni hayo yatalipwa ambayo yanatokana na kodi ya ardhi, kumekuwepo na madeni mengi ya 3bn/- na kuendelea, Mheshimiwa Naibu waziri wa ardhi alipokuja alisema tuhakikishe kwamba wanalipa kodi ya ardhi,” amesema.

Amesema aliwaita ili kuwaelimisha na kuwapa taarifa ikiwemo kuwapa ‘notice’ ya kulipa na kumaliza madeni yao. “Na watu kweli wamekiri na wamefanya ‘commitment’ kwamba wataenda kulipa kodi zao katika nafasi mbalimbali. Taasisi za serikali, taasis za dini, wafanyabishara na watu binafsi, na makapumbi wamekubali kulipa madeni yao kwa mda mfupi,” amesema.

Kyobya amesema kuwa anategemea wadaiwa wataweza kulipa madeni yao kwa mda mfupi huku akitoa wito kwa Manispaa ya Mikindani ihakikishe inarekebisha mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya ardhi ili kuepuka mkanganyiko wa ukusanyaji wa kodi za ardhi.

“Lakin pia nimetoa wito kwamba manispaa ihakikishe inarekebisha mfumo wa ukuanyaji wa kodi ya ardhi kusiwe na ‘duplication’, ---yaan kila mtu aweze kulipa kile anachodaiwa kwa sababu baadhi ya ‘data’ ilikuwa inaonyesha kwamba kuna mtu anadaiwa kodi kwenye kiwanja ambacho sio cha kwake,” amesema.

Lakin pia amewataka kuhakikisha kwamba wanahamasisha wale waliotelekeza viwanja wanaenda kusafisha viwanja vyao ambavyo wameviach ili visiwe vichake.

Kwa upande wake Mkurungezi wa Manispaa ya Mikindani Kanali Emmanuel Mwaigobeko amesema taasisi za serikali na za dini zinaongoza kwa kuwa na madeni makubwa ukilinganisha na watu wengine.

“Taasis za serikali zinadaiwa pesa nyingi na taasis za dini. Taasis za dini ambazo ni kama 40 na za dini 30 zote kwa ujumla zinadaiwa 1.7bn/-. Wengi wameahidi kwamba watalipa, wengine mpaka kufika tarehe 30 mwezi huu,” amesema na kuongeza taasis hizo zimeahidi kulipa kidogokidgo na kwamba mkapa kufikia mwezi wa 6 mwaka huu watakuwa wameshamaliza madeni hayo.

Amesema kutolipa kodi hiyo kwa wakati inaathiri utendaji wa serikali katika kutoa huduma ambapo fedha hizo hutegemewa katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya (kulia) akiongoza kikao cha wamiliki mbalimbali wa ardhi Manispaa ya Mtwara Mikindani ili kujadili namna Bora ya kulipa malimbikizo ya madai ya kodi ya ardhi. Kushoto ni Mkurungezi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Kanali Emmanuel Mwaigobeko.


baadhi ya wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi Manispaa ya Mtwara Mikindani
DC wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2