GAMBO AAHIDI KUFUATILIA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA BARABARA YA BARACUDA-SORENYI KATA YA BARAA | Tarimo Blog






MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo ameendelea na ziara yake mtaa kwa mtaa ya kusikiliza kero za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na Mamlaka husika, ameyasema hayo wakati akitembelea Kata ya Baraa.

Akiwa katika ziara hiyo Mbunge amewaahidi wananchi wa Kata hiyo kuwa atakuwa mstari wa mbele na kutumia nguvu kubwa kuhakikisha  barabara ya Barakuda Soreni ambayo imekuwa kero sana kwa wakazi wa mtaa huo nakusababishia kukosa baadhi ya huduma za kijamiii inatengenezwa na mamlaka husika.

Gambo ameendelea kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Jimbo la Arusha pamoja na kueleza mambo makubwa ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  Rais DR. John Pombe Joseph Magufuli tangu achaguliwe mwaka 2015.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2