Na Jusline Marvo -Arusha
Diwani wa kata ya Sekei wa halmashauri ya jiji la Arusha Gerald John Sebastian amewataka wananchi kuishi katika mfumo ambao hayati Dkt.Magufuli ameuacha na kuleta nidhamu kwenye kila sekta ambapo amewasihi kuishi katika yale mema aliyoyafundisha.
Akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha,Sebastian amesema pamoja na kimaendeleo aliyoyafanya hayati Dkt.Magufuli ameleta nidhamu makazini.
“Hayati Dkt.Magufuli pamoja na kutuongoza katika mambo mema,ametufanya watanzania tuheshimike na kuthaminiwa ndani na nje ya nchi yetu,” Alisema Sebastian.
Aidha amesema kuwa katika miaka mitano iliyopita Mikoa mingi imekua kiuchumi, miundo mbinu na katika huduma za kijamii tofauti na miaka ya nyuma ilivyokuwa ambapo kwa sasa miundombinu ya barabara inaendelea kujengwa.
“Amefanya uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja kuimarika,lakini tunamshukuru Mumngu kwa kutupa kiongozi mwenye maono makubwa ya nchi yake."Alieleza Sebastian.
Pamoja na hayo amewataka watanzania kutokuwa ma wasiwasi na Rais wa aeamu ya sita Mhe.Samia Suluhu Hassan kwani katika kazi alizofanya katika bunge la katiba na kufanya kazi na hayati Dkt.Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wawe na imani na yeye.
Diwani wa kata ya Sekei wa halmashauri ya jiji la Arusha Gerald John Sebastian akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa qa Arusha .
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment