Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasilisha Bungeni jina la aliyekuwa Waziri wa Fedha Philip Mpango kuwa Makamu wake wa Rais.
Jina hilo limepelekwa leo Machi 30 mwaka huu asubuhi saa 10:45 ambapo jina hilo lilipelekwa na Rais kwa Spika wa Bunge kupitia Msaidizi wake ADC ambaye aliwakilisha jina hilo kwa Spika.
Akizungumza leo Bungeni, asubuhi, Spika wa Bunge Job Ndugai aliwaambia wabunge kwamba Rais Samia Suluhu Hassan tayari amependekeza jina la Makamu wa Rais baada ya kushauriana na Chama chake na sasa anawasilisha Bunge ili kupitishwa na Bunge.
Spika Ndugai alimuita Msaidizi wa Rais kuja kuleta nyaraka ambayo iliyokuwa kwenye bahasha ambalo ndimo lilikuwemo jina la Dk.Mpango.Kabla ya kulisoma jina hilo wabunge walikuwa na hamu kubwa ya kutaka kufahamu ni jina gani ambalo limepitishwa.Baadae Spika Ndugai akataja jina la Dk.Mpango.
"kabla hajaondoka naomba niangalie kama kuna sehemu ya kusaini hii nyaraka,"alisema Spika na kisha kumuita Katibu wa Bunge na baada ya kushauriana alimruhusu ADC aondoke. "Kabla ya kuondoka naomba niseme tu huyu ni ADC wa kwanza mwanamke katika nchi yetu.
"Nimepokea nyaraka hizi, mpelekee salamu zetu za upendo, ahsante sana .Wabunge bahasha ya kwanza ni hii na bahasha ya pili ni hii nyeupe, naomba nisome jina ambalo limependekezwa na Rais wetu kwa ajili ya Makamu wa Rais.Jina ambalo nalisoma hapa ambalo nimeletewa ni Dk.Philip Mpango."
Baada ya kusoma jina hilo, Spika Ndugai alitoa ufafanuzi kwamba ili jina hilo lipitishwe na Bunge linahitajika kupata kura za wabunge asilimia 50.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment