Na John Nditi, Morogoro
MSANII wa Muziki wa Hip Hop na Bongo Flava kutoka mkoani Morogoro, Seleman Msindi au maarufu Afande Sele amemtaja aliyekuwa Rais wa Tanzania , Dk John Magufuli , kuwa alitaka keki ya Dunia igawanywe sawa kwa sawa bila ya upendeleo .
Pia ametoa wito kwa viongozi wanaokuja na waliopo wavivae viatu vya Dk Magufuli kiukweli na si kiunafiki kwani wapo baadhi ya viongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikalini waliona alikuwa anawabana.
Licha ya baadhi ya viongozi pia wapo baadhi ya matajiri kwa upande wao nao walimchukia kutokana na uamuzi wake wa kuwatetea watu wanyonge ,kwani siku zote matajiri wanapenda kuwatumia watu wanyonge kama mtaji wao .
Afande Sele , alibainisha hayo wakati akizungumza na Gazeti hili jana mara baada ya kutokea kwa kifo cha Rais Dk Magufuli , mnamo Machi 17, mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Alisema baada ya kutokea kwa kifo cha Dk Magufuli kwa sasa haioni kesho ya Tanzania na Afrika kwa ujumla ikiwa na maisha ya baadaye ya watoto wetu yatakuwa wapi.
Msindi , kimuziki amewahi kushinda tuzo ya mkali wa rhymes mwaka 2003 kutokana na wimbo yake wa "Darubini Kali" akiwa na makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori', yaliyokuwa na makazi yake mjini Morogoro.
Hivyo alisema Watanzania waliomba na kusali sana kwa zaidi ya miaka 30 ili waweze kumpata Rais ambaye atawatetea watu wanyonge na baada ya kumpata na katika muda mfupi Rais wetu ameondoka kwa mapenzi ya Mungu huyo huyo .
Msanii huyo , alisema ; “ Kuondoka duniani kwa Rais Magufuli ni pigo kwa wale mama mtilie , wamachinga, na watu wanyonge wan chi hii watarudi kwenye unyonge wao huwenda kwa haraka sana kwa sababu sioni mtu atakaye vaa viatu vya Magufuli sasa ,sawa akisema hiki acha bila kurubuniwa au kununuliwa …kuondoka kwake ni kurudi nyuma” alisema Afande Sele.
Machi 15, 2018 Afande Sele alitangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) mbele ya Rais Dk Magufuli kwa lengo ka kuunga mkono jitihada zake anazozifanya katika kupigania na kukiomba chama kimpokee kama kijana wao.
Afande Sele alieleza hayo wakati alipokuwa anatumbuiza muziki kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro walioweza kuhudhuria shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha Sigara mkoani humo na Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi. Naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi naomba nikuhakikishie kwamba leo hii kutoka kwa dhati ya moyo wangu nimeamua nisimame upande mmoja na wewe ili nisiachwe katika maendeleo” alisema Afande Sele.
Msanii wa muziki wa Hip Hop na Bongo Flava kutoka mkoani Morogoro, Seleman Msindi au maarufu Afande Sele alipotangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Chama cha ACT - Wazalendo Machi 15, 2018 mbele ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hayati Rais Dk John Magufuli kwa lengo ka kuunga mkono jitihada za Rais wakati alipozindua kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro ( Picha na Maktaba yetu ) .
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment