Na Charles James, Michuzi TV
HATUTOMUONA tena! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuagwa leo na viongozi wa serikali pamoja na wananchi wake wa Chato ambao amewatumikia kwa takribani miaka 26.
Dk. Magufuli ambaye alifariki Machi 17 mwaka juu ameagwa katika uwanja wa mpira wenye jina lake na sasa kinachosubiriwa ni kesho kuzikwa ambapo mazishi hayo yataongozwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Dk Magufuli amekua mtumishi wa Wananchi wa Chato kwa miaka 26 ambapo alianza kama Mbunge wao mwaka 1995 na alidumu kwenye nafasi hiyo hadi mwaka 2015 alipoamua kugombea Urais.
Wananchi wa Chato watamkumbuka mambo mengi ikiwemo kwa ujenzi na Daraja la Busisi, Mahakama ya Wilaya ya Chato, Vituo vya Afya na Elimu bure ambapo serikali ya Dk. Magufuli ilitoa fursa kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi kidato cha nne kusoma bila kulipa ada.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment