*Ni Mawasiliano ya Mkongo wa Taifa pamoja mawasiliano ya simu kuanzia 3G
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv - Tanganyika
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amesema kuwa bandari ya Kalema inayojengwa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi pindi inapokamilika inahitaji kuwa mawasiliano ya mkongo wa Taifa kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano hapo.
Kundo ameyasema hayo wakati wa ziara ya kuangalia hali ya Mawasiliano katika Mkoa wa Katavi kwa kufika katika Bandari ya Kalema kuona fursa za kuweka mawasiliano kutokana huduma nyingi zitakuwa za mtandao.
Amesema kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ikiwemo ujenzi wa bandari kwa kodi za wananchi hivyo kila sehemu inahitaji kuwa na mawasiliano yenye ubora.
Naibu Waziri Kundo amesema kuwa sehemu zote ambazo zinahitaji kufanyiwa maboresho zifanyiwe kazi sio za kuandika bila utekelezaji.
"Tunahitaji kufanya kazi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kuweza kupata maendeleo katika kutimiza ndoto ya Rais Daktari John Pombe Magufuli ya kuanzisha Wizara mpya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari"amesema Mhandisi Kundo.
Aidha amesema kabla ya serikali kwa upande wa Ziwa Tanganyika na Wilaya ya Tanganyika ilikuwa haina mvuto wa kibiashara lakini sasa kumegeuka fursa kwa kampuni za mawasiliano kuwekeza pamoja na minara iliyojengwa kuongeza uwezo wa 3G ili kuweza kutumia data.
Mhandisi Kundo amesema kuwa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo zinatakiwa kufanya kazi pamoja na kuwa wabunifu wa kutatua changamoto za wananchi na wale wanaofanya biashara wafanye kiushindani kwa kuzalisha.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi ,Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amesema kuwa ziara ya Naibu Waziri imejibu changamoto za mawasiliano pamoja na elimu ya kazi ya Wizara hiyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment