Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Simba wameendeleza ubabe ndani ya dimba la Benjamini Mkapa baada ya ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan.
Mchezo huo wa Kundi A umechezwa majira ya saa 10 alasiri ikishuhudiwa na watu wachache baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF kuzuia mashabiki kuingia uwanjani.
Katika mchezo huo ulichukua dakika 18 kwa Luis Miquisson kuandika bao la kwanza akimalizia pasi ya Benard Morrison na kuipa uongozi Simba.
Simba iliendelea kulisakama lango la Al Merrikh na kupitia kwa Beki wa kushoto Mohamed Hussein akaweza kuiandikia Simba goli la 2 na hadi wanakwenda mapumziko Simba wakiongoza kwa 2-0.
Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi kila upande ikitaka kufunga, dakika ya 50 Chriss Mugalu anaiandikia Simba goli la 3 na kuzamisha mwiba wa mwisho kwa wanamsimbazi hao na kupeleka kilio zaidi kwa wa sudani.
Hadi dakika 90 zinamalizika, Simba waliibuka na ushindi wa goli 3-0 wakiongoza kundi A kwa alama 10 wakifuatiwa na Al Ahlywenye alama 7.
Katika mchezo mwingine wa Kundi A, Al Ahly wameweza kuibuka na ushindi wa alama 3 ugenini baada ya ushindi dhidi ya As Vita baada ya kuwafunga goli 3-0.
Michezo ya kundi A itaendelea tena April 2, Simba wakiwakaribisha As Vita katika dimba la Benjamin Mkapa na Al Ahly wakiwa ugenini nchini Sudan.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment