Akizungumza jijini Dar es Salaam Kevala amesema hana shaka na utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mchapakazi wa kweli na kwamba yeye na kampuni yake wataendelea kusimama pamoja naye wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake.
" Kwanza kabisa tunampa pole kwa msiba wa mtangulizi wake sote tunaamini kuwa hayo yote ni mapenzi ya Mungu ...nasi tumepokea kwa masikitiko kama ilivyo kwa watanzania wote na ulimwengu kwa ujumla." amesema Kevela.
Amesema watanzania wanaamini chini ya uongozi wa Mama Samia Tanzania itazidi kupiga hatua za kimaendeleo huku akiwataka wasaidizi wake wa ngazi zote kumuunga mkono.
Amesema endapo watendaji hao waliopo chini yake watatimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ni wazi watakuwa nguzo nzuri kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa.
Amesema nyota njema huonekana tangu asubuhi na kwamba hata utendaji wa kazi wa Rais ulionekana tangu akiwa na nyadhifa zingine ndani ya Serikali tofauti na hiyo ya ngazi ya juu aliyonayo hivi sasa.
" Rais alishajipambanua katika utawala ndani miaka mingi, ameshashika nafasi za juu katika Serikali ikiwemo ya Makamu wa Rais, Waziri katika Serikali ya awamu ya nne na hata Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, uzoefu wake unamtosha kuliongoza Taifa hili" amesisitiza Kevela.
Amesema hatua ya yeye kuwa Rais wa Taifa hili kwa kiasi kikubwa kumeweza kuionyesha Dunia na ulimwengu mzima kuwa Tanzania ni nchi isiyokumbatia masuala ya mfumo dume unaotoa fursa kwa jinsia moja kushika nyadhifa ya juu ya uongozi.
Amesema hatua hiyo pamoja na kupokelewa vyema na wananchi wote zaidi kumewaheshimisha wanawake nchini na dunia nzima na kumuona kama mfano kwao katika jitihada za kujiletea maendeleo.
"Tunamuombea kwa Mungu aweze kumpa ulinzi wa kutosha na afya njema wakati wote ili aweze kutekeleza ipasavyo majukumu ya kututumikia wananchi wake." amesema Kevela.
Amesema Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ipo katika mikono salama na zaidi akawaomba wananchi kumuunga mkono kwa kuchapa kazi bila kuchoka ili kulisukuma mbele Taifa la Tanzania.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment