Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni amewataka wananchi kupunguza ulevi huku akizuia kutolewa kwa vibali vya matamasha ya burudani[disko] katika kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli.
Marufuku hiyo ameitoa akiwa kata ya Igwachanya katika mkutano wa maombolezo ya msiba wa na kwamba kitendo cha kufanya matamasha ya burudani na ulevi wa kupindukia havitavumiliwa katika kipindi hiki cha siku 21 za maomboleza ya msiba wa kitaifa.
"Itatushangaza sana tunalia kilio kikubwa hivi halafu watu kwenye baa wanapiga 'Ndomboloo ya Solo' inamaana wewe hauko pamoja na sisi Naelekeza tupiga nyimbo za maombolezo na tupunguze ulevi, Hakuna vibali vya disco vitakavyotolewa kwa kipindi hiki tutakuwa tumekiuka taratibu"Alisema Dc Kanoni
Awali katibu tawala wa wilaya ya Wanging'ombe Edward Manga amesema kuwa mchango wa Magufuli katika taifa hili umekuwa wa kuigwa barani Afrika kwani amefanikiwa kuifikisha nchi katika uchumi wa kati kabla ya wakati uliopangwa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Agnetha Mpangile amesema pigo lililowakuta watanzania la kuondokewa na Rais Magufuli halitosahaulika huku viongozi wa dini akiwemo Mbaraka Thabiti Sheikh wa wilaya hiyo wakisema watanzania hatupaswi kukata tamaa kwani maandiko yanasema baada ya kifo cha mussa alitumwa Joshua kwenda kuwafikisha wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi.
Baadhi ya wakazi wa Wanging'ombe akiwemo Aiden Valanzi na Erasto Homange wamesema kifo cha Magufuli kimewagusa sana kwa kuwa aliwatetea sana wanyonge.
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment