Jane Edward,Michuzi TV,Arusha.
Baadhi ya Wafanyabiashara Mkoani Arusha ,wameeleza kuwa namna bora ya kumkumbuka aliyekuwa Rais Hayati John Magufuli ni kwa kufanya kazi na kuyaenzi aliyoyafanya wakati wa uongozi wake katika kuwajali wananchi wanyonge.
Mmoja wa wafanyabiashara hao,Mustafa Janoowalla kutoka kampuni ya Royal Safety iliyopo mjini hapa alisema kuwa,Hayati Rais Magufuli alikuwa akipambania maslahi ya wananchi bila kujali kabila lolote kikubwa ni kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mtu.
Mustafa alisema kuwa,Rais Magufuli atakumbukwa kwa maswala mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya ikiwemo kuleta ndege ya ATCL ambayo kama nchi tunajivunia uwepo wa ndege zetu wenyewe kuliko kutegemea uwepo wa ndege kutoka nchi zetu.
Naye Balozi mdogo wa Burundi hapa Arusha, Leonidas Mbakenga alisema kuwa,watamuenzi Hayati Rais Magufuli kwa namna ambavyo aliweka nchi pazuri Sana na kuibadilisha katika sekta mbalimbali.
Mbakenga alisema kuwa,kuna miradi katika serikali ya Hayati Rais Magufuli ambapo kulikuwepo na mpango wa kujenga reli ambapo alikuwa anaboresha mambo ya usafiri Sana hivyo waafrika wanaomboleza wote hakuna aliyetegemea kifo kama hicho kitatokea.
Alisema kuwa,Rais mpya mama Samia Suluhu Hassan ajipe moyo maana mipango yote ya serikali walikuwa wanafanya pamoja miradi aliyokuwa anafanya Hayati Rais Magufuli ataweza kuifanya na kuiboresha ili watanzania waendelee kuwa na matumaini ya kwamba huko mbele ni kuzuri.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment