WAOMBOLEZAJI WAMUIMBIA DK.MAGUFULI HIVI ...MTETEZI WA WANYONGE...MTETEZI WA WANYONGE...MTETEZI WA WAWANYONGE | Tarimo Blog


 Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MTETEZI wa Wanyonge ,mtetezi wa wanyonge ...mtetezi wa wanyonge...mtetezi wa wanyonge! Hayo ndio maneno yaliyokuwa yakisikika kutoka kwa wananchi waliokuwa unje ya wa Ndege wa Terminal I jijini Dar es salaaam.

Wakati nyimbo hizo zikiendelea kumuelezea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk .John Magufuli baadhi ya waombolezaji waliokuwa maeneo hayo walikuwa wamepatandika kanga chini kama ishara ya upendo wakati wakisubiria mwili kufika uwanjani hapo.

Huzuni,majonzi simanzi ndizo ambazo kwa sehemu kubwa zilikuwa zimetawala muda wote lakini hawakukosekana waliokuwa wakitoa ujumbe wa nyimbo za kumsifu na kumpongeza Dk.Magufuli ambapo mbali ya kusikika wakisema ' Jembe Letu' .

Misururu ya watu katika barabara ya kuelekea uwanjani ilikuwa imetanda pande zote za barabara huku vilio vikiwa vimetawala.Hakika ni majonzi makubwa ambayo Taifa la Tanzania limeyapata kutokana na kifo cha Dk.Magufuli.

Aidha waombolezaji wengine waliamua kushika maua na miti kwa ajili kumuagia Dk.Magufuli na kutoa heshima za mwisho na kumuaga.Upendo wa Watanzania kwa Dk.Magufuli umeoneshwa kwa vitendo, watu wamuamua kukaa barabarani ,pamoja na mvua walibaki wakimsubiri.

Michuzi TV na Michuzi Blog imeshuhua namna ambavyo wananchi wa Dar es Salaam ambavyo walihakikisha wanapata nafas ya kuaga mwili wa Dk.Magufuli.Hakika kwa idadi ya watu ambao wamejotokeza haijapata kutokea, watu ni wengi kila kona .Ni majonzi,ni simanzi tu.

Wakati kukiwa na maelfu ya watu barabarani ,vyombo vya ulinzi na usalama navyo villikuwa imara kuhakikisha watu wote wanakuwa salama, hakuna madhara yoyote yanayoweza kutokea kwa waombolezaji.













 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2