Na Jusline Marco-Arusha
Wawakilishi wa Wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wametoa salam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,Mhe Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa wawakilishi wa wanajeshi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,Kanali Rafael Kiptoo akisaini kitabu cha maombolezo amesema kuwa Hayati Rais Dkt Magufuli alikuwa ni tegemeo katika kukuza maendeleo ya jumuiya.
"Kwa kweli tulishtushwa na kusikitishwa kufuatia taarifa zilizotufikiwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Dkt John Magufuli kilichotangazwa na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan ambaye kwa sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita."Alisema Kanali Kiptoo
Aidha amesema kuwa kwa niaba ya wanajeshi wa jumuiya ya Afrika Mashariki hayati Dkt.Magufuli alikuwa amiri jeshi mkuu na alikuwa kipaumbele katika safari ya kuendesha jumuiya hiyo tangu ilivyozinduliwa hapo awali.
"Hayati Dkt.Magufuli alikuwa kielelezo na shujaa wa wengi hasa kwetu sisi kama wanajeshi na tutaendelea kumuenzi kwa vitendo na kwa kazi zetu zote,tunalikumbuka pia taifa na familia kwa wakati huu mgumu na majonzi"alisema Kanali Kiptoo
Ameongeza kuwa wataendelea kuiombea nchi ya Tanzania na Jumuiya nzima amani na utulivu wakati huu wa maombi na maombolezo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment