KAMPUNI ya itel inayojishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki imemtangaza rasmi Diamond Platnumz kuwa balozi wake.
Katika taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa instagram katika page ya itel Tanzania imeeleza kuwa wamefurahi kumkaribisha Diamond Platnumz kuwa balozi wa itel.
“Leo ni siku maalum! Tunayo furaha kubwa kumkaribisha Diamond Platnumz balozi wetu mpya wa itel.” Imesema sehemu ya chapicho hilo.
Moja ya post iliyopostiwa ukurasa wa instagram @iteltanzania yenye picha ya Diamond Platnumz akiwa ameshika simu ya itel A37.
Kwa upande mwingine Diamond amethibitisha pia katika chapisho lake la ukurasa wa instagram kuwa sasa ni rasmi amekuwa balozi wa itel.
“Najivunia sana kuungana na timu ya itel na pia nina furaha kuwajuza kuwa, sasa ni Balozi wa bidhaa za itel” imesema taarifa hiyo.
Post aliyotumia Diamond Platnumz kutangaza kuwa sasa ni balozi wa itel.
Wakati huohuo itel imeitambulisha simu yake mpya ya itel A37 ambayo imeingia hivi karibuni sokoni, simu hiyo yenye HD+waterdrop full screen inatarajiwa kuuzwa kwa bei nafuu zaidi ili kumsaidia kila Mtanzania kumiliki smartphone.
Itel A37
Kwa Taarifa zaidi tembelea kurasa za itelTanzania instagram na Facebook au bofya hapa: https://www.instagram.com/iteltanzania/
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment