Charles James, Michuzi TV
WABUNGE watatu walioteuliwa jana na Rais Mama Samia Suluhu Hassan wameapishwa bungeni leo na Spika wa Bunge, Job Ndugai ili kuanza rasmi majukumu ya kuitumikia nafasi zao kikatiba.
Wabunge hao watatu waliopishwa leo ni Balozi Dk Bashiru Ally, Balozi Liberata Mulamula na Mbarouk Nassor Mbarouk. Katika watatu hao waliopishwa, Balozi Mulamula yeye pia aliteuliwa pia kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Naibu wake Mbarouk Nassor Mbarouk.
Akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge hao, Spika Ndugai amewapongeza wabunge hao walioteuliwa huku pia akiwapongeza mawaziri walioteuliwa na kuaminiwa na Rais Mama Samia na kuwataka kuwatumikia watanzania kwa uzalendo.
Spika Ndugai amesema mawaziri hao walioteuliwa wanapaswa kutambua kuwa nafasi walizopata ni nzuri lakini wanapaswa kutambua kuwa Bungeni ndio sehemu haswa ya kwao.
" Niwapongeze mawaziri lakini niwatake mkafanye kazi ipasavyo, inashangaza kuona wananchi huko mtaani wanalalamika, ukikaa na wafanyabiashara huko wanauliza huyo Waziri wa Uwekezaji na Biashara yupo wapi? Unashangaa Tamisemi ambayo ndio yenye wananchi haitekelezi vizuri majukumu yake huko kijijini.
Mfano Wizara ya Afya inashangaza kuona madawa hospitalini hayapo, niwaombe mkajitahidi kufanya kazi kubwa na kumsaidia kazi Rais Mama Samia ambaye amewaamini ili wote tukatekeleze Ilani yetu tuliyoinadi vema, " Amesema Spika Ndugai.
Ameitaka Wizara ya Ardhi kuajiri wataalamu wa kupima Ardhi ili kuifanya sekta hiyo kupata mapato yanayotokana na Ardhi.
Balozi Liberata Mulamula
Balozi Dk Bashiru Ally akiapa kuwa Mbunge
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment