BAADA YA MAKISATU KUFIKIA TAMATI, WIKI YA UBUNIFU KUANZA DAR MEI 17 HADI 22 | Tarimo Blog

 

KUFUATIA maonesho ya MAKISATU jijini Dodoma kufika tamati leo, Mei 11, 2021,  maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Tanzania sasa kufanyika Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine 7 ambayo ni Mwanza, Zanzibar, Morogoro, Iringa, Mbeya, Tanga, Arusha.

Katika taarifa iliyotolewa na Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano kutoka Mfuko wa Ubunifu wa Mendeleo ya Watu (HDIF), Hannah Mwandoloma iliyotolewa leo Mei, 11, 2021 imesema kuwa maonesho hayo yataanza Mei 17-22, 2021 jijini Dar es Salaam.

 Kaika maonesho hayo wadau mbalimbali wa ubunifu watajumuika pamoja wakiwemo mashirika binafsi, wadau wa maendeleo, watunga sera, wataalam mbalimbali, wasomi pamoja na wabunifu ili kujadiliana na kubadilishana ujuzi kuhusiana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Ubunifu kwa Uchumi wa Kidijitali Stahimilivu na Jumuishi”

Kwa Dar es Salaam wiki hiyo itafanyika katika kumbi za LAPF Tower, Makumbusho.

Taarifa hiyo imewaomba wadau wote wa ubunifu wanaaswa kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho hayo ili kujadili mijadala mbali mbali  ambayo pia itarushwa kwa njia ya redio, runinga na mitandao ya kijamii.

Wiki ya Ubunifu Tanzania imeandaliwa UKaid kupitia Mfuko wa Ubunifu wa Mendeleo ya Watu (HDIF),  kwa ushirikiano na Costech na UNDP, wadau mbalimbali  kwa udhamini mkubwa wa Vodacom, NMB Bank, European Union, UNCDF, Tigo, Ubalozi wa Netherlands, CRDB Bank, UNICEF, Segal Family Foundation, Ubalozi wa Uswizi, Ifakara Innovation Hub na UNWomen.

Unakumbushwa kuzingatia umbali kati yako na mwingine, kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2