GRACE MUGABE ADAIWA KUKIUKA TARATIBU ZA KUMZIKA MUMEWE | Tarimo Blog



Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

CHIFU Zvimba ambaye ni kiongozi mkuu wa kitamaduni wa kijiji cha aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemuandikia waraka mke wa Hayati Mugabe Bi. Grace Mugambe na kumtaka kufika katika mahakama ya kitamaduni Alhamisi wiki ijayo kwa madai ya kutofuata taratibu za kitamaduni wakati wa kumzika kiongozi huyo. 

Grace Mugabe aliyeondoka nchini humo kwenda Singapore mapema 2020 anadaiwa kumzika kiongozi huyo katika makaburi ya familia kinyume na tamaduni ya jamii yao ambayo ilichagua kumzika katika sehemu aliyozikwa Mama yake pamoja na jamaa zake wa karibu.

Kwa mujibu wa jarida la The East Africa imeelezwa kuwa ujumbe huo uliotumwa na Chifu Zvimba pia umemtuhumu Grace kwa kuacha mali za Hayati Mugabe zilizotapakaa nchini humo na  kumuelekeza Grace kuufukua mwili wa hayati Mugabe ili uzikwe tena kwa kufuata utamaduni wa watu wa Zvimba na hiyo ni pamoja na kulipa faini kwa kutoa mbuzi na ng'ombe wawili.

Robert Mugabe alifariki dunia Septemba 6, 2019 nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu na hiyo ni baada ya miaka miwili tangu aondolewe madarakani na jeshi baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 37 na alizikwa Zvimba kilomita tano kutoka mji mkuu Harare.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2