MALIPO HAFIFU YACHANGIA KAZI ZA SANAA KUSHUKA | Tarimo Blog

Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
SERIKALI yaja na mpango wa bei elekezi ya kuuza kazi za Sanaa.

Akizungumza na Waandishi Wahabari Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk Kiagho Kilonzo katika hafla ya uzinduzi wa tamthilia ya ‘We Men’ amesema wazo hilo limeibuka Mara baada ya wasanii hao kwa muda mrefu kila mmoja kuwalipwa anavyojisikia na wakati Mwengine malipo mengine hayaendani na kazi husika wanazozifanya.

“ Wasanii wetu wanatakiwa kunufaika na kazi zao maana ndio kiinua mgongo chao au jasho la kazi zao."

Kilonzo ameongezea kuwa wakati Mwengine wasanii wanafanya kazi huku malipo hayaendani na gharama za uandaaji wa filamu

"Kwa hali hiyo inawavunja moyo sana wasanii na watayarishaji kutokana na malipo yake hayafiki hata robo."

Hata hivyo Kilonzo ameweka wazi wazi hilo la serikali kuja na bei elekezi ambayo haitaumiza upande wowote.

Pia ameeleza kwa sasa ipo haja ya kuboresha maisha ya wadau hawa kwa kuboresha masoko na kuimarisha vyama vyao ambapo tayari viashiria vya kuelekea huko vimeanza kuonekana.

"Ongezeko la watazamaji wa kazi za filamu na kutolea mfano tamthiliya ya Juakali imepata tuzo ya tamthiliya bora nchini Zambia, jambo linaloonyesha namna gani tamthiliya za kitanzania zinatazamwa."


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2