MSALABA MWEKUNDU KITETO WACHANGIA DAMU | Tarimo Blog

Na Mwandishi wetu, Kiteto

Ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito wanaopoteza maisha kwa kukosa damu salama, chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, wametoa msaada wa kibinadamu kwa kuchangia chupa 14 za damu salama.


Pia wamekabidhi vifaa vya usafi kwenye zahanati ya Ndaleta, msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasio na uwezo shule ya msingi Ndaleta na kuhamasisha jamii kuchimba vyoo na kuvitumia.

Lengo la msaada huo ni kusaidiana na Serikali kuhudumia jamii ambayo imekuwa na changamoto mbalimbali za kibinadamu na kuhamasisha jamii kuchimba vyoo na kuvitumia kuepuka magonjwa ya milipuko.

Mkuu wa kitengo cha habari na maafa wa Msalaba Mwekundu Mkoa wa Manyara, Mohamed Hamad amesema hatua hiyo imelenga kumuenzi mwanzilishi wa shirika hilo lililoanzishwa mwaka 1863.

"Tuna wajibu wa kumuenzi mwanzilishi wa Msalaba Mwekundu duniani Henry Leonard kwa kutoa misaada ya kiutu ambapo yeye pamoja na kutoa misaada kwa wahanga wa vita aliandika pia kitabu kuhusiana na maafa yaliyotokana na vita vilivyosababisha watu wengi kupoteza maisha," amesema.

Mratibu wa damu salama Priscal Likiliwike amesema hospitali ya Wilaya ya Kiteto ina uhitaji mkubwa wa damu salama kwani kuna wanaopoteza maisha haswa wanawake wajawazito na watoto kwa kukosa huduma hiyo.Amesema Serikali inatambua mchango wa chama cha Msalaba Mwekundu ulimwenguni na hasa Kiteto katika kuwahudumia wananchi.

Amesema Msalaba Mwekundu Kiteto imefanya mambo mengi ya kimaendeleo kama vile masuala ya maji, afya, misaada ya kibinadamu, ukarabati wa mabwawa, ugawaji wa mbegu za mahindi na majani kwa mifugo, chakula cha mifugo na elimu ya kukabiliana na majanga.

Ofisa Tawala wa wilaya ya Kiteto, Musa Waziri ameipongeza Msalaba Mwekundu kwa kuendelea kuwa kisaidizi cha serikali na kuokoa maisha ya watu kwa kutoa misaada ya kibinadamu.

Chupa 14 za damu zilipatikana ambazo zitaokoa maisha ya wananchi hasa wajawazito ambapo baadhi ya wachangiaji wa damu hiyo Charles Kaaya, Abell Simba na Amina Abdalla wamesema lengo kubwa ni kusaidia jamii kama mwasisi wa shirika hilo alivyofanya.


 

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2