NMB yatoa milioni 150 washindi wa Bonge la Mpango | Tarimo Blog

BENKI ya NMB imetoa zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 150 kwa washindi wa prmosheni ya Bonge la Mpango, weka Ushinde inayolenga kuhamasisha watanzania kujiwekea akiba kupitia benki hiyo.

Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Janeth Shango amesema hayo jana mkoani hapa wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaji za miguu mitatu kwa mshindi wa promesheni hiyo Wilayani Masasi ambapo pia alishiriki na kushindanisha droo ya mwezi iliyofanyika katika tawi la benki hiyo Masasi.

Amesema toka promosheni hiyo ianze, Benki imetoa zawadi za pesa taslimu, bajaji zenye magurudumu matatu na gari aina ya Tata maarufu kama Kirikuu kwa washindi ambao ni wateja wao walioweka pesa katika akaunti zao kipindi cha kampeni ya promosheni hiyo inayoendelea nchi nzima kwa sasa.

“Vyote hivyo ambavyo tumeshatoa mpaka sasa tangu droo imeanza ni zaidi ya shilingi milioni 150 imetolewa,” amesema na kuongeza kuwa shilingi milioni 550 zinatarajiwa kutolewa kwa wateja wote watakaoshinda katika promosheni hiyo.

Katika droo ya mwezi iliyochezeshwa Masasi, Shango amesema washindi 10 walijishindia pesa taslimu na wateja wawili wengine walijishindia bajaji ya miguu mitatu na mshindi mmoja ambaye amejishindia gari aina ya Tata (Kirikuu).

Katika hatua nyingine, Shango alikabidhi bajaji ya miguu mitatu kwa mteja wao Wilyani Tandahimba ambaye alishinda bajaji ya miguu mitatu yenye thamani ya shilingi 4.5m/-. Pia alikabidhi mteja mshindi mwingine Wilayani Masasi ambaye alijishindia Bajaji ya miguu mitatu Masasi.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi bajaji kwa mshindi wa Masasi, Shango amewaomba wananchi wa Masasi, na Mkoa wa Mtwara nan chi nzima kushiriki kuchangamkia fursa hiyo ya promosheni ya weka ushinde kwa kuendelea kuweka hela katika akaunti zao za NMB, na ambao hawana akaunti kufungua ili kujishindia zawadi hizo zinazotolewa.

“Kwa hiyo ndugu wananchi watanzania, naomba niwaalike muweze kujishidnia zawadi mbalimbali ambazo benki yenu nzuri imeitoa kama kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii lakani pia mpango wake wa kuendeleza utamaduni wa kujiwekea akiba kwa wananchi wote, karibuni sana,” amesema.

Amesema mchezaji ambaye anaingia katika droo ya NMB ni mteja yeyote ambaye ana akauti NMB, ana uwezo wa kuweka shilingi 100,000/- na kuendelea na yule anayetaka kufungua akaunti katika benki hiyo.

“Zawadi kubwa benki imetoa gari la kifahari aina ya Toyota Fortuna  lenye thamani ya shiling milioni169 kwa hiyo ni nafasi ya kipkee kabisa kumiliki gari,” amesema.

Mkulima aliyeshinda kirikuu, Hamisi Zuberi, Mkazi wa kijiji cha Malamba, wilaya ya Tandahimba ameshukuru Benki ya NMB kwa kuwanzisha promosheni hiyo ambayo imepelekea yaye kujishindia bajaji ambayo itamsaidia katika shughuli zake za kilimo.

“Naishukuru sana Benki ya NMB, mimi ni mteja wao wa siku nyingi sana na nimekuwa nikitumia benki hiyo sio tu kwenye kuweka pesa lakini pia kupata ushauri mbalimbali katika shughuli zangu za kilimo, wamekuwa msaada mkubwa sana katika kuweka hela na kuzitumia vizuri,” amesema.

Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango (Kulia) akikabidhi zawadi ya Bajaji ya Miguu Mitatu yenye thamani ya shilingi  milioni 4.5 Kwa Mshindi ya Bonge la Mpango Hamisi Zuberi Mkazi wa  Tandahimba, Mkoani Mtwara.
Meneja wa Kanda akikabidhi Janeth Shango (Wa Tatu kulia) akikabidhi Bajaji Kwa mshindi wa Bonge la Mpango kutoka Wilaya ya Masasi Zakaria Masije

Wafanyakazi wa Tawi la NMB na makao Makuu na Meneja wa Kanda ya Kusini Janet Shango (wa 4 kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Bajaji ya Miguu Mitatu (Katikati ameketi kwenye Bajaji) Hamisi Zuberi mara baada ya hafla ya kukabidhiwa Bajaji hiyo
Hamisi Zuberi (nyuma,) akisepa na Bajaji yake huku ikiendeshwa na ndugu yake ambaye jina lake halikufahamika.
Zakari akizungumza baada ya kukabidhiwa Bajaji yake
Wafanyakazi wa NMB Tawi la Masasi na wengine kutoka makao Makuu na Meneja wa Kanda Janeth Shango wakiwa kwenye picha ya pamoja na Zakaria Masije mkazi wa Masasi aliyeshinda Bajaji huku wakifurahia na wakazi wa Masasi
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2