Mufti wa Tanzania amesema Sala ya Eid kitaifa itasaliwa Viwanja vya Mnazi Mmoja na Baraza la Eid litafanyika Ukumbi wa Karimjee ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.
Aidha Mhe. Mufti amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge kwa kuona umuhimu wa kufutarisha Wananchi wa Makundi mbalimbali Jijini humo ambapo amesema kitendo hicho ni sadaka njema mbele za Mungu.
Akizungumza Katika hafla hiyo, RC Kunenge amewashukuru Wananchi walioitika wito wake kwa kujitokeza kwa wingi kuungana nae Katika futari huku akitoa shukrani za dhati pia kwa Wadau walioshirikiana nae kufanikisha Jambo hilo.
Tukio la Iftar ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ilifanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee na kushirikisha mamia ya wananchi wa Dar es salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment