RC MAKALLA AMALIZA MGOGORO WA MEYA NA MKURUGENZI KINONDONI | Tarimo Blog








MKUU wa mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla amemaliza sitofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza Kati ya Meya manispaa ya kinondoni  Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa Spora Liana.

Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao cha pamoja kilichoitishwa leo  na mkuu wa Mkoa  na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni.

Makalla amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2