Na Farida Mangube.
Vyombo vya habari vya Mtandaoni na Waaandishi wa Habari Nchini WAMETAKIWA kufuata misingi, kanuni, Sheria na maadili ya uandishi wa habari katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya kupashana habari mbalimbali, ili kuondokana na mikanganyiko inayoweza kujitokeza baina ya vyombo vya habari na Taasisi mbalimbali nchini.
Wito huo umetolewa katika mafunzo ya Waandishi wa Habari za Mtandaoni (Online Media) yalioandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadam yenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kufanya kazi zao kwa weledi kwa kufuata misingi ya Sheria ya Uandishi wa Habari
Akizungumza katika Mafunzo hayo leo 10 Mei, 2021. Mratibu wa Taifa Mtandao huo Onesmo Ole Ngurumwa amesema vyombo vya habari vya mtandaoni vinatakiwa kufuata Sheria na kuacha kufanya Kazi kwa mazoea.
"Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo vyombo vya Habari vya Mtandao, ili muweze kufanya kazi zenu vizuri za kuhabarisha umma na unaposema matumizi ya mtandao unazungumzia uhuru wa kujieleza" amesema Onesmo.
Aidha ameongeza kuwa ni muhimu vyombo vya habari vya Mtandao vikasimama vizuri na kuwa wanataaluma wazuri ambao watazingatia misingi, Sheria, kanuni na taratibu za taaluma ya Uandishi wa Habari katika utaekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile amewaomba THRDC kuviwezesha vyombo vya Habari vya Mtandao kuwa uchumi unaotengamaa kwani vingi havina mipango ya biashara (Business Plan) huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuwa na hali ya kujijali wao wenyewe wawapo kazini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment