WASANII WASHAURIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI | Tarimo Blog


Baadhi ya wadau  na wasanii wakiwa katika uzinduzi wa Ukumbi wa Starehe Mrina park Bagamoyo.
Baadhi ya wasanii walioshiriki  wasanii  walioshiriki uzinduzi wa Ukumbi Starehe  wa Mrina park Bagamoyo.
 

Na Mwandishi Wetu.

WASANII Nchini Tanzania wametakiwa kuendelea kujituma na kufanya kazi zao kwa weledi zaidi lengo likiwa ni kuendelea kujulikana ndani na nje ya Nchi ili mziki wao uweze kwenda mbali zaidi huku wadau wakiahidi kuwa nao bega kwa bega. 

Wito ulitolewa  na  Fredrick Mramba wakati wa uzinduzi wa eneo Jipya la Burudani maarufu kama New Rafiki Mrina Mramba Park, uliofanyika huko Bagamoyo eneo la Mapinga siku ya Idd Mosi wakati akizungumza na wasanii hao pamoja na wageni waliofika kwenye tukio hilo.

Mrambaambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa New Rafiki Mrina Mramba Park aliwaasa wasanii mbalimbali waliokuwa wamejaa katika uzinduzi huo na kusema kuwa yeye aliona upo umuhimu wa kuwaalika wasanii hao akiwa kama mdau  ili waweze kukutana na wadau wengine na kubadilishana nao mawazo lakini pia kuweza kutumbuiza nyimbo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa eneo hilo jipya la burudani. 

Kwa upande wake, mgeni mwalikwa kutoka Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi Charles Sabiniani maarufu (Lowasa), aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwaunga mkono wasanii Nchini ili kazi zao zisonge mbele zaidi na hasa wasanii ambao bado ni wachanga.

"Ninaamini wapo wadau watakao ona umuhimu wa kuwainua wasanii chipukizi lakini pia tunamshukuru Mkurugenzi Mramba kwa kuona umuhimu wa kuwaalika wasanii hawa ili kuungana nao kwenye uzinduzi huu pamoja na kuwapa kipaumbele cha kutumbuiza,"alisema

Wakizungumza na Globu ya jamii kwa nyakati tofauti akiwemo Mshindi wa Bongo Star Search 2019 Meshaki Fukuta maarufu kama Meshamazing, wamewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono hasa pale wanapotaka kutoa nyimbo zao wanazokuwa wameziandaa.

Meshamazing alisema wao wakiwa wasanii nchini wamekuwa wakipata faraja pale wadau wanapoonesha kuwapa ushirikiano kama alivyofanya Mkurugenzi wa New Rafiki Mrina Mramba Park, Fredrick Mramba.

"Unajua hapa tumealikwa kwenye uzinduzi huu hasa ikizingatiwa leo ni Sikukuu, tutaimba tutaonesha makeke yetu na kama inavyojulikana kwamba wasanii tuna ushawishi mkubwa kwenye jamii hivyo tunaamini baada ya hapa tunaweza kupata saport kutoka kwa wadau mbalimbali," alisema.

Saimon Ally maalufu kama Green Boy, msanii wa Bongo Fleva takribani kwa miaka minne, alisema pamoja na kwamba wasanii wanapitia changamoto mbalimbali lakini wanatakiwa kupambana na kuhakikisha mziki unasonga mbele na kwamba amefanikiwa kutoa nyimbo nne ukiwemo ule wa chuchumaa, moja namba, Ng'adhaghila na mekapu.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2