Watoto 3000 Jijini Tanga kupewa majaribio ya sayansi ili kuwaandaa kuwa wabunifu | Tarimo Blog

 Raisa Said,Tanga.

Jumla yaWatoto  3000 wenye umri kwanzia miaka mitatu  wa Jijini Tanga wanatarajiwa kupewa mafunzo mbalimbali ya Kisayansi kwa vitendo kwa lengo la kuwaanda kuwa wabunifu wakubwa wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika  siku ya ubunifu iliyofanyika katika viwanja vya Kituo kipya cha  Sayansi kilichopo Kisosora jijini Tanga, Meneja wa Kituo hicho Gibson Kawago alisema watoto hao wakipewa elimu hiyo ya sayansi itawasaidia katika maisha yao ya badaye.

Kawago alieleza kwamba watoto waliolengwa ni watoto kuanzia miaka mitatu mpaka saba na kuendelea ambapo aliongeza ubunifu ni sayansi hivyo watoto wakijengwa wakiwa wadogo itawaongezea ujuzi na kujitambua .

Meneja huyo alisema kuwa kituo hicho kimejengwa kwa ajili ya watoto na vijana kwa ajili ya kujifunza majaribio mbalimbali ya sayansi , teknolojia na hesabu ili kuwajenga kuona sayansi ni kitu rahisi .

Alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi waache kuwapeleka watoto wao katika kuogelea na michezo mingine badala yake wawapeleke katika kituo hicho ili waweze kupata ujuzi wakiwa na umri mdogo kwa kufanya majaribio mbalimbali ya kisayansi na teknorojia.

Alifafanua kuwa kitu kilichowasukuma kuanza kuwafundisha watoto wenye umri huo ni msukumo uliokuwepo wakati walipokuwa na mradi wa kuzunguka kwenye shule za msingi zilizopo jijini hapa katika wiki ya afrika ni sayansi iliyofanyika mwaka jana

Aidha alisema kuwa  wiki  hiyo ya ubunifu inakwenda sambamba na kauli mbiu ya   “ubunifu kwa uchumi wa kidigital stahimilivu na jumuishi” ambapo alisisitiza ubunifu unahusisha na  mambo ya sayansi, teknolojia na hesabu .

Aliongeza kuwa wiki ya ubunifu ilianza kuadhimishwa mwaka 2015 na lengo ni kuwasaidia wabunifu kuonyesha bunifu zao.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa alisema kituo hicho ni muhimu na kwamba kitawasaidia watoto na vijana katika mafanikio yao.

Hatahivyo, Mwilapwa alitumia fursa hiyo kuwataka wabunifu watumie wiki  hiyo kujifunza zaidi na kuboresha ubunifu wao

Meneja wa kituo kipya cha Sayansi  Gibson Kawago akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Tanga  Thobias Mwilapwa


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2