WATOTO 62.993 KUPATA USAJILI WA VYETI VYA KUZALIWA JIJI LA ARUSHA | Tarimo Blog

Na.Vero Ignatus,ARUSHA

Zaidi ya Watoto 62,993 wanategemewa kusajiliwa katika mpango wa usajili wa vyeti vya kuzaliwa chini ya miaka mitano jijini Arusha,ambapo zaidi ya wasaidizi wa usajili 306 wamepatiwa mafunzo ,jumla ya vituo 94 vimetengwa kwaajili ya zoezi hilo ,vituo 25 kati ya hivyo ni ofisi za watendaji kata,69 ni vituo vya tiba

Akizungumza katika uzinduzi wa zoezi hilo Mratibu wa mpango huo wa usajili Martha Gorge alisema kuwa tangia kuanza kwa zoezi hilo siku ya kwanza 11mei 2021,walifanikiwa kusajili Watoto 2,119 sawa na 3.4%,hadi kufikia mei 18 mwaka huu jumla ya watoto 19.034 sawa na 30.2% wamesajiliwa na kupata vyeti vyao vya kuzaliwa, ambapo jumla ya Watoto 43,959 hawajasajiliwa ambao nis awa na 69.7%

Alisema kuwa utekelezaji wa mpango huo ni kwa mujibu wa sheria ya usajili wa vizazi na vifo,uwakala umepewa mamlaka ya kusajili vizazi au vifo vilivyotokea Tanzania bara,na mpango huo unalenga kusajili watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano, ndani ya muda maalum kwa kuweka mfumo wa usajili wa vizazi ndani ya siku 90 tokea tukio litokee.

Kwa upande Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt.John Pima alisema kuwa mpango huo wa kusajili watoto chini ya miaka mitano, umeanzishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kupitia wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ikishirikiana na wadau wa maendeleo ,ambao ni shirika la Umoja wa Mataifala kuhudumia Watoto Duniani UNICEF

Alisema kuwa mpango huo ni moja ya hatua zilizochukuliwa na serikali ili kukabiliana na changamoto za zinazopelekea usajili kuwa chini, kutokana na uelewa mdogo kuhusu umuhimu wa usajili wa kizazi na kuwa na cheti cha kuzaliwa,umbali wa ofisi ya usajili na makazi ya wananchi ambapo ipo ofisi kuu ya wilaya,tozo pamoja na sababu nyingine ambazo kwa ujumla zimesababisha wananchi wengi kukosa nyaraka hiyo muhimu ya utambulisho ambao ni cheti cha kuzaliwa.

Dkt.Pima alisema ili mtoto asajiliwe anatakiwa mzazi au mlezi kulwa na kiambatanisho kimojawapo ,kama kadi ya kliniki ya mama/mtoto,cheti cha ubatizo,kitambulisho cha taifa Nida,barua ya uthibitisho kutoka kwa mtendaji wa Kijiji/mtaa,inayothibitisha majina kamili ya mtoto ,mahali alipozaliwa na tarehe ya kuzaliwa

Aidha Pima ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Arusha ,kuhamasishana na kupeana tarifa wao kwa wao ili kuhakikisha kuwa wanapata cheti cha kuzaliwa kwani ni muhimu, na kinatumika mahali popote katika nchi hii ya Tanzania, na faida zake ni nyingi,haswa kwaajili ya takwimu muhimu kwa taifa.

Nae mganga mkuu kutoka Jiji la Arusha Kheri Kagya alisema. zoezi hilo ni fursa kwaajili ya watu wote ambao hawajasajiliwa, kwani ni muhimu mno,na vinatolewa katika kata,zahanati za serikali ,mashirika ya dini,na vyeti hivyo ni halali na vinatambulika sehemu yeyote katika nchi ,hivyo wananchi waondokane na dhana potofu na Jiji limetenga siku 12 kwaajili ya zoezi hilo baada yah apo zoezi litaendelea katika vituo vya kutolea huduma za afya na zoezi litakamilika tarehe 26/ 5/2021

Kagya alisema lengo ni kuhakikisha tukio la kizazi linaandikishwa mahali lilipotokea kwa wakati Pamoja na kuondoa limbikizo kubwa ya Watoto ambao hawajasajiliwa aidha amewataka wazazi kutokuwanyima Watoto haki yao ya msingi ya kusajiliwa.

''Mtoto anastahili cheti cha kuzaliwa mpe haki yake ‘’
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima akikata utepe ishara ya uzinduzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano Jijini Arusha,kushoto kwake ni mganga mkuu wa Halmashauri ya Arusha Dkt Kheri,akifuatiwa na Diwani wa katabya Levolosi Kamili.Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano Jijini hapo
Mganga mkuu wa jiji la la Arusha Kheri Kagya akizungumza katika uzinduzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano Jijini Arusha.
Msajili wa vyeti H/C Hosiana Joseph Nassary ,akimsajili mtoto chinibya miaka mitano Jijini Arusha Kama inavyoonekana katika Picha.Kutoka kushoto Msajili wa vyeti Levolosi H/C Suzan Mpelembwa akiendelea kuwahudumia Wazazi waliokuja na. Watoto katika maeneo ya Soko la Kilombero Jijini Arusha.
Kikundi Cha ngoma kutoka daaraja mbili wakitumbuiza katika uzinduzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano Jijini Arusha.Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.John Pima akionyesha kitabu Cha usajili Mara baada ya kukata utepe katika uzinduzi rasmi wa usajili wa mtoto chini ya miaka mitano
Mratibu wa Mpango wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano Jijini Arusha Martha George akizungumza katika uzinduzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano
Muwakilishi kutoka Rita Getrude Pius akizungumza katika uzinduzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano Jijini Arusha katika viwanja vya Soko la Kilombero kata ya Levolosi.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.John Pima akimkabidhi mmoja wawazazi cheti Cha kuzaliwa Mara baada ya kukamilisha usajili wa mtoto.





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2