MASHINDANO YA 'KAZI IENDELEE CUP' YAZINDULIWA JIJINI DAR | Tarimo Blog






Diwani wa Kata bya Buguruni Busolo Pazi akisalimiana na wachezaji wa Netiboli mara baada ya kuzindua mashindano hayo.
Diwani ya Kata ya Buguruni Busulo Pazi (katikati,) akisalimia na viongozi mbalimbali mara baada ya kuzindua mashindano hayo.



Mashindano yakiendelea.


MASHINDANO maalumu ya mpira wa Netiboli  yanayolenga kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yamezinduliwa leo jijini Dar es Salaam kwa timu nne kati ya 25 kutimua vumbi katika viwanja vya shule ya Msingi viziwi Buguruni,  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mashindano hayo diwani ya kata ya Buguruni Busolo Pazi amesema, mashindano hayo yamelenga kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan vilevile yamelenga kukuza na kuinua vipaji kwa mchezo huo wa Netiboli katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Pazi amesema, kupitia mashindano hayo wachezaji watadumisha ushirikiano pamoja kushirikishana fursa mbalimbali kwa kuwa michezo ni ajira.

Akizungumza kwa niaba ya taasisi ya Furahika Education College David Msuya amesema timu 25 za Netiboli kutoka Mkoa wa Dar es Salaam zenye kuhamasisha uzalendo zimeshiriki mashindano hayo yatakayofanyika kwa siku 5.

Amesema kuwa taasisi hiyo imeendelea kuiunga mkono serikali kupitia sera ya elimu na michezo mashuleni na kupitia mashindano hayo washindi watapata nafasi ya kujishindia fedha taslimu na vikombe vya ushindi.

Kwa upande wake katibu wa Chama cha Netiboli Dar es Salaam (CHANEDA,) Joseph Stanslaus amesema mashindano hayo yamehusisha timu za kada mbalimbali ikiwemo afya, jeshi na magereza ambako ni chimbuko la mchezo huo.

Pia amewataka wadau kujitokeza kudhamini mchezo huo wa Netiboli kwa kuwekeza katika vifaa vya michezo na viwanja vya michezo.



 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2