MWENGE WA UHURU MANYARA NA MIRADI 29 YA ZAIDI YA BILIONI 6 | Tarimo Blog

Na Gift Thadey, Manyara

Mwenge wa uhuru umeingia Mkoani Manyara na unatarajia kukagua, kutembelea, kuona na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 29 yenye thamani ya shilingi bilioni 6.6.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere, akizungumza mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakati akipokea mwenge wa uhuru kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai, amesema utakimbizwa kwa kilomita 1,089.3.

Makongoro amesema mwenge huo utaweka mawe ya msingi ya miradi 10 ya thamani ya sh3.7 bilioni na kuzindua miradi minne ya thamani ya sh342.3 milioni. Amesema utafungua miradi mitatu ya thamani ya sh534.3 milioni na kukagua na kuona miradi 12 ya thamani ya sh2 bilioni. 

“Mwenge wa uhuru utakimbizwa kwenye tano za Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang’ na Mbulu, kisha kuukabidhi mkoa wa Arusha Juni 16,” amesema Makongoro. Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula, amesema mwenge wa uhuru utatembelea, kukagua na kuona miradi sita ya gharama ya shilingi 239, 159, 539.10. Mhandisi Chaula amesema mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Simanjiro, utakimbizwa kwa kilomita 139. 

Mwalimu wa mazingira wa shule ya Sekondari Mgutwa, Exaud Mafie amesema mradi wa mazingira
uliozinduliwa na mwenge umegharimu sh16.7 milioni. 

Mafie amesema katika mradi huo, shule ya Mgutwa imechangia sh8.8 milioni, Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro sh1.6 milioni, Malihai club sh125,000 na Maivaro Ever Green sh6 milioni. Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, Josephine Mwambashi amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni Tehama ni msingi wa Taifa endelevu itumie kwa usahihi na uwajibikaji.


……………………………………………………………………………….


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2