PSPTB YAJIPANGA KUHUDUMIA WANANCHI KWENYE MAONESHO YA SABASABA | Tarimo Blog

 

Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo lililo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na PSPTB katika kipindi hiki cha Sabasaba ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali  kuanzia ngazi ya chini mpaka  ile ya juu pamoja na usajili wa wanachama.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Shamim Mdee amesema wanatoa huduma zote ikiwemo jinsi ya kujisajili kufanya Mitihani, malipo ya Ada kwa Wanataaluma, ametoa wito kwa wote wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya PSPTB kufika katika Banda lao lililopo ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Amesema Bodi hiyo kwa sasa mfumo wa kidijitari wa kutoa huduma zake hususan usajili wa wanafunzi na Wananchama kupitia tovuti yao, amesema huduma hizo zinapatikana hata ukiwa sehemu mbalimbali pia kwa sasa huduma hizo zimehamia Sabasaba.
Wafanyakazi wa Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakiongozwa na Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Shamim Mdee wakiwa kwenye picha ya pamoja katika banda la Bodi hiyo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2