RAIS SAMIA AWANYOOSHEA KIDOLE CCM KUHUSU MICHEZO | Tarimo Blog


Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Samia Suluhu Hassani ameagiza sekretarieti ya CCM Kuboresha Viwanja vyote vya michezo vinavyomilikiwa na chama hicho kwa kuwekwa nyasi bandia.

Rais Samia amesema hayo leo mapema jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na Vijana katika mkoa wa Mwanza wakiwawakilisha vijana taifa.

Rais Samia amesema kuwa serikali imeondoa tozo ya VAT kwa nyasi Bandia zote zinaingizwa nchini ili kutoa fursa kwa uendelezwaji wa sekta ya michezo ambayo ni kama sehemu kubwa ya ajira kwa Vijana.

“Hapa nizungumze na chama changu cha Mapinduzi (CCM), Viwanja hivi vinamilikiwa na chama changu CCM Lakini hali yake airidhishi sasa fursa imetoka niombe sana, Viwanja vitengenezwe viwekwe nyasi bandia ili Vijana wetu watumie Viwanja hivi na wajiendeleze kimichezo lakini walipe thamani ya ile pesa wanayoitoa kutumia Viwanja hivi hivyo basi namtaka Naibu katibu mkuu ambaye upo hapa kuandaa program ya kuboresha Viwanja hivi.” Amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kama CCM awana uwezo wa kukarabati Viwanja hivyo itafute wawekezaji hili kufanya maboresho ya Viwanja hivyo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2