RC MAKALLA AZITAKA HALMASHAURI KUJIEPUSHA NA HATI CHAFU. | Tarimo Blog

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinafanya shughuli kwa Weledi ili kuepuka kashfa za Hati Chafu au Hati za Mashaka kutoka kwa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali CAG.

RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao Cha Baraza la Madiwani Ilala kilichoketi Leo kupitia Ripoti ya CAG ambapo amesema ni vyema Halmashauri hizo zikawapatia ushirikiano wa kutosha Wakaguzi kwa kuonyesha vielelezo vinavyohitajika.

Aidha RC Makalla ameipongeza Manispaa ya Jiji la Ilala kwa kupata Hati Safi kwa miaka mitano mfululizo na kuitaka ifanyie kazi Maelekezo na Maagizo yaliyotolewa na CAG na Kamati ya Kudumu ya Bunge huku akiwataka kuwatumia vizuri Wakaguzi wa ndani.

Pamoja na hayo RC Makalla amewataka Madiwani kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miradi inaendana na thamani ya pesa.

Hata hivyo RC Makalla ametaka Watumishi wote waliosababisha dosari wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria pasipo uonevu.




 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2