RC TABORA AWAHIMIZI WAFANYABIASHARA MNADANI IPULI KUCHUKUA TAHADHARI YA KUJIKINGA NA COVID 19 | Tarimo Blog


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa pili kutoka kushoto)akipata maelezo kutoka Mfanyabiashara wa Nyama za kuchoma Simon Henerico wakati wa ziara yake kukagua ukusanyaji wa mapato na tahadahri zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa tatu kutoka kushoto)akipata maelezo kutoka Daktari wa Mifugo Mkoa wa Tabora . Dkt. Robert Machibya wakati wa ziara yake jana ya kukagua ukusanyaji wa mapato na kuangalia tahadhari zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa tatu kutoka kushoto)akiangalia ng’ombe wa mbegu kutoka Biharamulo ambazo zilikuwa zikiuzwa wakati wa ziara yake kukagua ukusanyaji wa mapato na kuangalia tahadhari zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa tatu kutoka kushoto)akipata maelezo kutoka Muuzaji wa Ng’ombe wa Mbegu kutoka Biharamulo , Bw. Haruna Mazoea(kulia aliyevaa kofia) wakati wa ziara yake kukagua ukusanyaji wa mapato na kuangalia tahadhari zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kulia)akizungumza jana na wafanyabiashara katika Mnada wa Ng’ombe wa Ipuli , Manispaa ya Tabora juu kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa pili kutoka kushoto)akitoa maelekezo jana kwa Daktari wa Mifugo Mkoa wa Tabora . Dkt. Robert Machibya( wa pili kutoka kulia) wakati wa ziara yake kukagua ukusanyaji wa mapato na kuangalia tahadhari zinachukuliwa dhidi ya virusi vya Corona katika Mnada wa Ipuli.

Baadhi ya ngo’mbe waliokuwa wakingonja kuuza jana katika Mnada wa Ipuli uliopo Manispaa ya Tabora.Picha na Tiganya Vincent


……………………………………………………………………………

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka wananchi na wafanyabiashara katika Mnada wa Ipuli kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona(COVID-19)

Alisema ikiwa nchini jirani zinakabiliwa na tatizo hilo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Tanzania akachukua hatua za kujikinga kama zinavyoshauriwa na wataalamu wa sekta ya afya.

Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo jana alipokuwa katika ziara ya kukagua ukusanyaji wa mapato na hatua zinazochukuliwa kwa wafanyabiashara wa ng’ombe , mbuzi na kondoo katika Mnada wa Ipuli uliopo Manispaa ya Tabora za kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.

Alisema ni lazima kwenye Minada na maeneo yanayokusanya watu wengi kama vile masokoni , Stendi ,mashuleni kukawekwa ndoo za maji tirikia , sabuni ili wanaofanya shughuli hapo waweze kunawa kila wakati.
Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza watu wote wanaoendesha shughuli za kujitafutia riziki katika Mnada wa Ipuli na maeneo yenye mikusanyiko kuvaa wakati wote barakoa na kutumia vitakasa mikono.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameiagiza Idara ya Afya ya Manispaa ya Tabora kuhakikisha inajenga vyoo na kuboresha hali ya usafi katika Mnada wa Ipuli ili kulinda afya za watu wanakwenda siku ya Jumamosi kupata nyama choma.

Alisema ya usafi katika Mnada huo hairidhishi na vyoo vilivyopo ni vichache ukilinganisha ya watu wanaokuwepo siku ya Jumamosi.

Aidha Balozi Dkt. Batilda aliwaahidi wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo kutatua matatizo yanayowakabili ikiwemo la baadhi ya watu kuziba njia ya kupeleka ng’ombe mnadani , ukosefu wa majosho, ukosefu wa nyasi za kisasa za kulisha mifugo na ukosefu wa mbegu bora za ng’ombe

Awali mfanyabiashara wa ng’ombe Haruna Mazoea alisema wamelazima kufuata ng’ombe wa mbegu kutoka Biharamulo mkoani Kagera na wengine nchini Rwanda kama njia ya kuboresha ng’ombe wa Tabora.

Alisema aina ya ngo’mbe kutoka Biharamulo wanafaida kwa kuwa ni wakubwa na wanauzwa kuanzia shilingi milioni 1.8 hadi 2 kwa mmoja.Mazoea aliiomba Serikali kuasaidia kuboresha aina ya ng’ombe Mkoani Tabora kwa kuwapa wafugaji mbegu bora za ng’ombe na kuwapatia mbegu za majani kupanda kwa ajili kulisha na kunenepesha mifugo wao ili waweze kupata bei kubwa.


Mkuu wa Mnada wa Ipuli katika Manispaa ya Tabora Freddy Newton alisema siku ya mnada wanapokea kati ya ng’ombe 200 hadi 250 na mbuzi 100 hadi 150.Alisema ng’ombe mmoja analipiwa ushuru wa shilingi 7,500/= na mbuzi 3,000/= ambapo Manispaa ya Tabora inachukua kwenye fedha hizo shilingi 1,500/= kwa ng’ombe na 500/= kwa mbuzi anayeuzwa.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Tabora ni mwendelezo wa ziara ambazo amezipanga za kukutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitatua ili kujenga Tabora mpya.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2