TALGWU kicheko tupu ni baada ya changamoto za watumishi kuzidi kutatuliwa na Rais Samia | Tarimo Blog

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

Uongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania  (TALGWU) mkoa wa Njombe umesema umefurahishwa na kupongeza uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua changamo za watumishi wa umma ikiwemo kupandisha madaraja kwa watumishi kwa zaidi ya 80%

Viongozi wa Chama hicho wamesema utatuzi wa changamoto hizo ni jitihada za serikali na Rais Samia kutokana na ahadi zake alizotoa hivi karibuni katika sherehe ya wafanyakazi iliyofanyika mkoani Mwanza

Hata hivyo wamesema kucheleweshwa  kwa maslahi ya wastaafu ambao walikuwa watumishi wa serikali pamoja na maslahi duni kuna zidi kuwapa hofu watumishi waliopo kazini hivi sasa huku mamlaka zinazohusika zikiombwa kuzifanyia kazi kwa haraka staiki za wafanyakazi.

Hayo yamebainishwa na wajumbe katika mkutano mkuu wa kawaida wa chama hicho mkoa wa Njombe, akiwemo Hellen Kalege na Siston Mizengo ambao wamesema licha ya jitihada zilizoanza kuchukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan juu ya kupandishwa madaraja kwa asilimia 80 hadi sasa lakini bado wastaafu wengi wamekuwa wakicheleweshewa mafao yao.

“Kikwazo kikubwa sana ni maslahi kwa wastaafu kutokana na kucheleweshewa sana lakini pia tunatarajia katika awamu hii Rais atarekebisha na tutalipwa kwa wakati”alisema Hellen Kalege

Katibu mtendaji wa TALGWU mkoa wa Njombe bwana Raymond Chimbuya amesema chama hicho kimeendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za watumishi kwa kuishirikisha serikali mara kwa mara ili kupata muarobaini huku wakiamini serikali hii ya awamu ya sita itazitatua kabisa changamoto zao.

“Lakini kwasababu serikali yetu ni sikivu,kama chama tumeendelea kutatua changamoto ya migogoro sehemu ya kazi zilizokuwa zinatokea na kwa kiasi kikubwa imepungua sana”alisema Raymond Chimbuya

Katibu tawala msaidizi sehemu za uchumi na uzalishaji mkoa wa Njombe Ayoub Mndeme kwa niaba ya mkuu wa mkoa amesema bado serikali inaendelea kushughulikia changamoto za watumishi kwani hakuna serikali imara bila wafanyakazi wanaotekeleza wajibu wao kwa amani na salama.

“Mnafanya kazi kubwa katika utekelezaji wa sera na mipango ya serikali,kuna mafanikio mengi kwa kwa kweli ambayo napaswa kutoa pongezi hasa kutoa elimu kwa wanachama na kutetea maslahi yao licha ya changamoto mbali mbali ambazo zinajitokeza”alisema Mndeme

Chama hicho katika mkutano wake unaofanyika mjini Njombe kinaendelea ikiwa kinatarajia pia kufanya uchaguzi kwa ajili ya viongozi wapya kwa miaka mitano.


Katibu mtendaji wa TALGWU mkoa wa Njombe bwana Raymond Chimbuya akisoma risala ya Chama hicho kwa mbele ya wajumbe na mgeni rasmi katika mkutano wa kawaida ulioambatana na uchaguzi

Baadhi ya wanachama wa TALGWU wakiwa kwenye mkutano na kusikiliza ajenda za kikao hicho zinazoendelea mkoani Njombe.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2