TANZIA; MHANDISI PATRICK MFUGALE AFARIKI DUNIA | Tarimo Blog

Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale amefariki dunia leo Juni 29,2021

Mfugale alizaliwa katika eneo la Ifunda, mkoa wa Iringa na 1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.


Alipata shahada ya kwanza ya uhandisi mwaka 1983 kutoka Chuo Kikuu cha Rokii (Uhindi) iliyofuatwa na shahada ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Loughborough (Uingereza) mwaka 1995.


Mwaka 2003 alipokea tuzo ya Bodi ya Wahandisi wa Tanzania na mwaka 2018 alipokea tuzo nyingine iitwayo "Engineering Execellency". Patrick Mgufale alitengeneza mfumo wa usimamizi madaraja uitwao "Bridge Management System."

Mfugale amefanikiwa kusimamia ujenzi wa baadhi ya madaraja yakiwemo
Daraja la Mkapa kwenye mto Rufiji, daraja la Rusumo mkoani Mara, daraja la Kikwete, kwenye mto Malagarasi, daraja la Nyerere Kigamboni na daraja la Kijazi lililopo ubungo Mkoani Dar es Salaam.

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa.

1977 Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi.
1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
1992 Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
1994-1995 Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza.

Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja hapa nchini.

Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System.

2014 Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.

Alitumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja hapa nchini.


Mfugale Alibuni daraja la Magarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.

Mfugale mpaka anafariki dunia alikuwa ni mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 hapa nchini.

Alikuwa ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa hapa nchini

Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.

2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2