TASAC YAKUTANA NA WADAU KUJADILI SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA MAJI | Tarimo Blog


Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

SHIRIKA la Wakala wa Meli nchini (TASAC) limesema kuwa litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi kwa kutoa huduma kwa usafirishaji wa shehena ndani ya nchi na nje ya nchi.

Akizungumza na katika mkutano wa wadau wa usafirishaji nje nchi na ndani ya nchi Mkurugenzi Udhibibiti Huduma za Usafiri  wa TASAC  Deogratius Mkasa amesema kuna umhimu wa kuwajengea uwezo wa wasafirishaji wa shehena katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo wanaweza kuzitatua.

Amesema kuwa elimu hiyo ni endelelevu wa wadau kwani baada ya kufanya jijini Dar es Salaam watakwenda katika mikoa ya Tanga na Arusha kwa kuweza kurahisisha mawakala wa usafirishaji wa shehena zza kwenda nje pamoja na za nje kuingia nchini.

Mkasa amesema wadau wakisikilizwa lazima kuwe na uwianio wakati Tasac itapotoa uandaji wa kanuni katika sekta hiyo

Mkurugenzi wa  Mkuu shirika la wasafirishaji wa Shehena ISCOST Daniel Kiangi amesema kuwa shirika hilo lina wanachama wa Nne ambao ni Tanzania ,Kenya ,Uganda na Zambia ambapo wamekuwa ana ushirikiano na vyombo vya udhibiti ikiwemo TASAC, Bandari pamoja na Mamlaka ya mapato Tanzania  (TRA).

Kwa upande wa  Mwenyekiti wa Baraza la Wasafirishaji wa Shehena kwa njia ya Maji Ashraf Ghan  amesema kuwa usafirishaji wa mizigio kwa njia ya maji unahitaji kuwa na elimu na sio kufanyika kwa holela.

Amesema kuwa kukaa pamoja na Tasac kunaleta afya katika kutatua changamoto ikiwa ni kupunguza kwa gharama kutokana na  kujua taratibu zilizowekwa kwa ndani na nje ya nchi pamoja na kufanya kazi kwa weledi kwa pende zote mbili za mdau na mdhibiti.

 

Mkurugenzi wa Udhibiti Huduma za Usafiri Majini wa Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) Deogratius Mkasa akizungumza katika mkutano wa wadau wa usafirishaji wa shehena wa ndani na nje nchi katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa ISCOST Daniel Kiangi akizungumza kuhusiana na wadau kushirikiana katika masuala mbalimbali katika kujenga kwa ajili ya maendeleo katika mkutano wadau wa usafirishaji wa shehena ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya wadau wakifatilia mada katika mkutano wa wadau wa usafirishaji wa shehena Ndani na Nje ya nchi katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa ushafirishaji wa shehena za ndani na nje ya nchi mara baada ya kufanya majadiliano katika sekta ya usafiri wa maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Huduma za Usafiri Majini wa TASAC Deogratius Mkasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo kukutana na wadau wa usafirishaji wa shehena ndani ya nchi na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Baraza la Usafirishaji wa Shehena ndani na nje ya nchi Ashraf Ghan akizungumza kuhusiana na ushirikiano na mamlaka za serikali katika kutimiza matakwa ya sekta a usafirishaji wa kwa njia ya maji katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.


 




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2