TAWA KUONGEZA IDADI YA WANYAMA RUHILA | Tarimo Blog

MAMLAKA ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(Tawa)imejipanga kuongeza idadi ya wanyama katika bustani ya wanyamapori ya Ruhila ilIyopo umbali wa km 8 kutoka Songea mjini kama mkakati wake wa kuvutia na kuongeza idadi ya watalii watakaofika katika Bustani hiyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Tawa Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko, wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Tawa waliotembelea katika Bustani ya Ruhila na maeneo yanayosimamiwa na Mamlaka hiyo ili kuboresha na kutumia vivutio vilivyopo kama sehemu ya kuingizia Serikali mapato.

Meja Jenerali Semfuko amesema, katika mkakati huo Tawa imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kujenga sehemu ya kuhifadhi wanyama wakali wakiwemo Simba na Chui ambao ni kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Jenerali Semfuko,wanyama wengine watakaongezwa kwenye Bustani hiyo ni pamoja na Twiga,Pofu,Swala,Pundamilia ambapo zoezi la kupeleka wanyama hao katika Bustani limeshaanza.

“tunataka kuona eneo hili linakuwa sehemu mojawapo ya kuvutia watalii katika ukanda wetu wa kusini mwa Tanzania,tutahakikisha tunaleta Wanyama mbalimbali ambao wataweza kuwavutia watu kuja katika eneo hili”amesema.

Aidha amesema, ili kufanikisha mpango huo amemuagiza Kamanda wa kikosi cha kuzuia Ujangili Kanda ya Kusini, kuangalia namna ya kushirikiana na wadau wengine kuja kuwekeza ili kuwavutia wananchi wengi kuja kufanya utalii.

Ametoa wito kwa Watanzania kufahamu kwamba Songea kuna eneo zuri la kuja kutalii na kuwekeza badala ya kwenda kwenye maeneo mengine ya nchi sambamba na kuviomba vya Habari kuhakikisha wanaitangaza Bustani ya Ruhila ili iweze kufahamika na watu wengi zaidi.

Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kusini Keneth Sanga amesema, kwa mwezi idadi ya watu wanakuja kutalii katika Bustani hiyo ni kati ya 30 hadi 40 na mwaka 200 hadi 300.

Amesema, kwa sasa kazi zinazofanyika katika Bustani ya Ruhila ni kuongeza wanyamapori wengi zaidi ili kuwavutia wageni wengi kuja kutembelea eneo hilo ambao zaidi ni Watanzania na wachache kutoka nje ya Nchi.

Amesema,Bustani ya Wanyamapori Ruhila ilianzishwa mwaka 1973 na kuwekewa uzio mwaka 1974 ikiwa chini ya usimamizi wa Mkoa wa Ruvuma mwaka 1992 ambapo majengo na eneo lote lilikabidhiwa chini ya usimamizi wa idara ya Wanyamapori.

Sanga amesema, ilipofika mwaka 1916 eneo limekabidhiwa chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(Tawa).

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2