TNRF YAPANDA MITI MLIMA SUYE | Tarimo Blog



Na.Vero Ignatus,Arusha

Jumuiko la Mali Asili Tanzania (TNRF) limeendelea kutunza mifumo ya ikolojia  ya asili katika kuijengea jamii uwezo kutoataarifasahihi ili wadau wa maendeleo ikiwemo serikali, pamoja na makundi mbalimbali ili kushiriki vema katika suala la uhifadhi mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupanda miti katika mlima Suye uliopo Kata ya Kimandolu jijini Arusha Mkurugenzi wa Jumuiko la Mali Asili Tanzania (TNRF) Bwana Zacharia Faustin amesema upo umuhimu mkubwa wa kuhifadhi na kutunza mazingira katika jiji hilo kwa kuwa ni jiji la kitalii.

Amesema jukumu la kuhifadhi mazingira ni la kila mmoja huku akimshukuru mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana John Mongela kwa kushirikiana  natimu ya viongozi wengine pamoja na wananchi kuwa mabalozi kupanda miti katika mlima Suye ambao ndiyo jicho la utalii kwa jiji la Arusha na kwamba ukiendelea kuwa na uasilia wake utakuwa kivutio kikubwa cha utalii na kuongeza pato la mkoa wa Arusha.

Amesisitiza jamii kuwa na utamaduni wa kushiriki katika uhifadhi wa mazingira kwa kupanda mitiili  kulinda misitu na kuhifadhivyanzo vya majia mbapo Jumuiko la Mali Asili Tanzania limepanda mitimingi ya mfano katika mlima Suye na tayari limesambaza na kupanda miti zaidi ya elfu kumi katika maeneo mbalimbali ambayo ni kame kama vile Ziwa Natron.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma Bwana Sambala Said amesema anashirikiana na uongozi pamoja na wananchi wa jiji la Arusha kuboresha mazingira ya mlima Suye, kuwa tayari kupokea watalii ili kurudisha uhai wa jiji la Arusha katika sekta ya utalii ambayo ni moyo wa Uchumi wa eneo la Ukanda wa Kaskazini kwani eneo la Kanda ya Kati pia linategemea maendeleo kupitia  utalii.

Aidha Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kaskazini Francis Nyamhanga ,amesema wananchi wanapaswa kutambua kuwa mazingira yao ni Maisha yao hivyo watumie nishati mbadala ili kulinda na kuongoa mfumo wa ikolojia katika hali yake ya asili.

Amesema kuwa jamiii inapaswa kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira, kutunza vyanzo vya maji huku wakizuia na kutotiririsha maji taka kwenye mito kwani kila mmoja ana jukumu la kutunza mazingira.

Zoezi la upandaji miti lilifanyika pia katika shule ya msingi Kimandolu ambapo kikundi cha vijana walio hitimu kidato cha sita ambao walitoa pendekezo la kupanda miti katika eneo la chanzo cha maji shuleni hapo walishiriki katika zoezi hilo kwa kupanda miti ya matunda na mbao  Zaidi ya 30 kwa lengo kuhamasisha vijana wengine kuwa na utamaduni huo ili kuendelea kutunza mifumo ya Ikolojia.

Kaulimbiu ya Kitaifa ya Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani  ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe juni 5 kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Tutumie Nishati Mbadala kuongoa/kurejesha Mifumo ya Ikolojia.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2