UVCCM DAR WAMLILIA HAYATI KAUNDA 'ALIKUA RAFIKI WA MWL NYERERE' | Tarimo Blog


Katibu wa Uhamasishaji Chipuki wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Mohammed Ummy akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa ubalozi wa Zambia nchini Tanzania mara baada ya kufika kwaajili ya kutoa salamu za rambirambi.
Katibu wa Uhamasishaji Chipukizi Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Mohamed Ummy akisaini kitabu cha maombolezo cha kifo cha aliyekua Rais wa kwanza wa Zambia, Kenneth Kaunda katika ubalozi wa Nchi hiyo jijini  Dar es Salaam leo.


KATIBU wa Uhamasishai Chipukizi Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Mohamed Ummy ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha aliyekua Rais na mpigania Uhuru wa nchi ya Zambia Hayati Kenneth Kaunda kilichotokea wiki iliyopita.

Ummy amesema Hayati Kaunda alikuwa rafiki mkubwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kupelekea mataifa yote kuwa rafiki na kuleta maendeleo ya watu.

Ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufika katika Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania kwaajili ya kutoa salamu za rambirambi kufuatia kwa msiba wa Hayati Kenneth Kaunda uliotokea hivi karibuni.

Amesema wao kama vijana wa CCM wamepokea kwa masikitiko kwasababu wameridhi historia ya nchi rafiki ya Zambia na Watanzania na matokeo yake   yanaonekana baada ya kuwepo kwa miradi ya maendeleo.

"Urafiki wao ndio ambao ulipelekea kuishawishi Taifa la China kuweza kujenga Reli ya TAZARA ambayo kwa mara ya kwanza ilitambulisha nchi ya China katika mataifa ya Afrika katika nyanja za uhandisi na kupelekea nchi ya China badala yake kuaminiwa katika zabuni mbalimbali na kuongeza mahusiano ya kidiplomasia na nchi za Afrika". Amesema Ummy.

Aidha Ummy amesema Hayati Mwalimu Nyerere na Kenneth Kaunda waliangalia katika karne ya 20 ni namna gani wanaweza kubadili dhana ya mataifa yao na watu wake kutoka katika dhana inayoegemea katika misingi ya kikabila kuja katika dhana ambayo inajielekeza katika Uchumi wa Maendeleo ya watu.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2