WANAFUNZI WA CHUO CHA DIPLOMASIA NA WAKUFUNZI WAO WATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI | Tarimo Blog

Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao wamefanya ziara ya mafunzo kwa kutembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma na kuzungumza na watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza namna Wizara watendaji wa Wizara wanavyotekeleza diplomasia ya uchumi kupitia kazi zao.

Wanafunzi hao kutoka kampasi ya Dar es Salaam na Dodoma walipata nafasi ya kusikiliza mada za muundo na majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wanachuo hao kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega aliwataka wanachuo hao kusikiliza kwa umakini mada zitakazotolewa na watendaji wa Wizara ambao wanafanya shughuli za kidiplomasia kwa vitendo ili kujiongezea ujuzi zaidi.

Balozi Anisa aliwaambia wanachuo hao kuwa Wizara inaona fahari kuwa na chuo hicho kwani kinawezesha upatikanaji wa elimu ya diplomasia kwa wananchi wengi na kuwataka wanachuo hao kuitumia elimu wanayoipata kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla

Akizungumza kukamilisha mazungumzo kati ya wanachuo hao na watendaji wa Wizara Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen Mbundi aliwataka wanachuo hao kuwa tayari na kujiandaa na dunia ya sasa ili waende na wakati uliopo na aliwaahidi kuwa Wizara iko tayari muda wowote kuwasaidia ili waweze kuitendea haki elimu waliyoipata.

Wanachuo hao na wakufunzi wao walikuwa na ziara ya siku mbili jijini Dodoma ambapo siku ya kwanza walienda kutembelea Bunge kwa mwaliko wa Naibu Waziri –Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Nassor Mbarouk na kujionea jisni Bunge la Tanzania linavyoendesha shughuli zake.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega akizungumza kuwakaribisha Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao waliotembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujifunza

Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akizungumza baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao waliotembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujifunza

Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) waliotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia (CFR) wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, walipowaongoza Wanafunzi wa kozi ya stashahada ya uzamili kutembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara

Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) walotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2